Askari Magereza wanaoshirikiana na wafungwa gerezani waonywa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema amewataka askari wa jeshi la magereza nchini kufanya kazi kwa weledi na ...


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema amewataka askari wa jeshi la magereza nchini kufanya kazi kwa weledi na kufata maadili ya kazi.

Waziri Mwigulu ameyasema hayo akifungua gereza la wilaya ya chato mkoa wa Geita. Ambapo alieleza kuwa kuna baadhi ya taarifa ya askari wanaokiuka maadili ya kazi na masharti ya wahalifu wawapo magerezani kwa kushirikiana nao kwa kuwapa simu na vitu vingine ambavyo ni kinyume cha sheria na maadili ya kazi yao.

Mwigulu ameongeza kusema kuwa kwasasa majira yamebadilika na aina ya Wahalifu wamebadilika ni wajibu wa askari kuzingatia maadili ya kazi kuliko walivyokuwa wakifanya zamani enzi watanzia wote wakiwa ndugu na wahalifu.

“Kuna taarifa za rejareja za baadhi ya magereza vijana wetu wanawapa simu wafungwa kuwasiliana na jamaa zao,zamani unaweza fikiria anasalimia familia lakini si sasa unaweza mpa simu kumbe anapanga mpango wa kuwateka hapo majira yamebadilika kwasababu sheria zipo basi tuzingatie sheria na maadili ya kazi zetu,”alisema Mwigulu.
Aidha Waziri Mwigulu ameongeza kusema kuwa wanajenga magereza kwajili ya kuwasaidia wale wanaopata matatizo lakini ndani ya mioyo yao wanatamani watu wasifanye makosa kupelekwa magerezani.


Kwa upande wake,Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk. Juma Malewa amesema kwasasa changamoto kubwa wanazokutana nazo baada ya kufungua gereza ni usafiri, upungufu wa askari hasa wanapofungua gereza jipya linaitaji askari wasiopungua 50 na changamoto nyingine ni miundombinu chakavu ya magereza na kumuomba waziri awasaidia kutatua changamoto hizo.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Askari Magereza wanaoshirikiana na wafungwa gerezani waonywa
Askari Magereza wanaoshirikiana na wafungwa gerezani waonywa
https://2.bp.blogspot.com/-mP3YmYjuE3o/WovqIkjoV_I/AAAAAAAACnI/xpYK57O02nAxb5bXLszlG-PBNt0CoG3zwCLcBGAs/s640/magereza.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-mP3YmYjuE3o/WovqIkjoV_I/AAAAAAAACnI/xpYK57O02nAxb5bXLszlG-PBNt0CoG3zwCLcBGAs/s72-c/magereza.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/askari-magereza-wanaoshirikiana-na.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/askari-magereza-wanaoshirikiana-na.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy