Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema amewataka askari wa jeshi la magereza nchini kufanya kazi kwa weledi na ...
Waziri Mwigulu ameyasema hayo akifungua gereza la wilaya ya chato mkoa wa Geita. Ambapo alieleza kuwa kuna baadhi ya taarifa ya askari wanaokiuka maadili ya kazi na masharti ya wahalifu wawapo magerezani kwa kushirikiana nao kwa kuwapa simu na vitu vingine ambavyo ni kinyume cha sheria na maadili ya kazi yao.
Mwigulu ameongeza kusema kuwa kwasasa majira yamebadilika na aina ya Wahalifu wamebadilika ni wajibu wa askari kuzingatia maadili ya kazi kuliko walivyokuwa wakifanya zamani enzi watanzia wote wakiwa ndugu na wahalifu.
“Kuna taarifa za rejareja za baadhi ya magereza vijana wetu wanawapa simu wafungwa kuwasiliana na jamaa zao,zamani unaweza fikiria anasalimia familia lakini si sasa unaweza mpa simu kumbe anapanga mpango wa kuwateka hapo majira yamebadilika kwasababu sheria zipo basi tuzingatie sheria na maadili ya kazi zetu,”alisema Mwigulu.
Kwa upande wake,Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk. Juma Malewa amesema kwasasa changamoto kubwa wanazokutana nazo baada ya kufungua gereza ni usafiri, upungufu wa askari hasa wanapofungua gereza jipya linaitaji askari wasiopungua 50 na changamoto nyingine ni miundombinu chakavu ya magereza na kumuomba waziri awasaidia kutatua changamoto hizo.
COMMENTS