Agrey Moris Aahidi Kuinyoa Simba SC

Ikiwa imesalia siku moja kabla ya Azam FC kupambana na Simba SC, nahodha msaidizi wa timu hiyo, Agrey Moris ameweka wazi kuwa hawataw...



Ikiwa imesalia siku moja kabla ya Azam FC kupambana na Simba SC, nahodha msaidizi wa timu hiyo, Agrey Moris ameweka wazi kuwa hawatawaangusha mashabiki kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo utakaopigwa kesho siku ya Jumatano majira ya saa 10.00 jioni, unatarajia kuwa mkali na wa aina yake kutokana na Azam FC iliyojikusanyia pointi 33 kuwa kwenye vita kali ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo dhidi ya wekundu hao walio kileleni kwa pointi 38.

Kupitia tovuti ya wana lamba lamba hao ya www.azamfc.co.tz, Moris aliwataka mashabiki kuondoa hofu na kuwaomba kujitokeza kwa wingi uwanjani kwenye mchezo huo ili kuwapa sapoti.
“Kwanza tunamshukuru Mungu wachezaji wako katika morali ya hali ya juu yaani inaonyesha kila mmoja anajiandaa kuhakikisha kutaka kushinda mchezo huu,” amesema.


Moris alikiri ushindani utakuwa mkubwa kutokana na Simba SC kuwa kileleni mwa ligi, na kudai kwa sasa timu yake imeongezewa morali kutokana na ushindi wa juzi walipoichapa Ndanda mabao 3-1.

“Hiyo inatupa morali zaidi ya kwenda kupambana kwa sababu sisi lengo letu ni kushinda mchezo huu kujihakikishia tunaifukuzia Simba katika nafasi ya juu,” alisema.

Tayari kikosi cha Azam FC kinachodhaminiwa na Benki ya NMB, Maji Safi ya Uhai Drinking Water na Tradegents, kilianza maandalizi juzi jioni kuelekea mchezo huo na wachezaji wakiendelea kukaa kambini tokea ulipomalizika mtanange dhidi ya Ndanda, yote hiyo ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuhakikisha inaibuka na pointi zote tatu.

Aidha itakumbukwa kuwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Azam Complex Septemba mwaka jana, timu hizo zilitoka suluhu.


Ushindi wowote wa Azam FC kwenye mchezo huo, utazidi kupunguza pengo la pointi baina yake na Simba na kufikia mbili na hivyo kuendeleza mapambano ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo, walioutwaa mara ya mwisho msimu wa 2013/2014.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Agrey Moris Aahidi Kuinyoa Simba SC
Agrey Moris Aahidi Kuinyoa Simba SC
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMMEzm1yIuMGWzyVV5ggcYbrtEUyVSfhSe_zbGj5Sl4gHdCnuoHy2lYk-tjbvwpocDsiSoGyu3PLMTke2XMjAjdxjoRZ2bz-j7qU6s7c1BtKTi-6jtrCUZJl1QfBRHOwrqzw7UJvxmNrDQ/s640/SC.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMMEzm1yIuMGWzyVV5ggcYbrtEUyVSfhSe_zbGj5Sl4gHdCnuoHy2lYk-tjbvwpocDsiSoGyu3PLMTke2XMjAjdxjoRZ2bz-j7qU6s7c1BtKTi-6jtrCUZJl1QfBRHOwrqzw7UJvxmNrDQ/s72-c/SC.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/agrey-moris-aahidi-kuinyoa-simba-sc.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/agrey-moris-aahidi-kuinyoa-simba-sc.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy