Msanii wa muziki kutoka nchini Rwanda, Muchoma ameendelea kuwa mfano bora kwa vijana waliopo katika mazingira magumu na waliokata tamaa ...
Msanii wa muziki kutoka nchini Rwanda, Muchoma ameendelea kuwa mfano bora kwa vijana waliopo katika mazingira magumu na waliokata tamaa ya kufanikiwa katika maisha.
Akiongea na Bongo5 msanii huyo ambaye pia anafanya muziki wa Singeli ameeleza kuwa licha ya kupitia maisha magumu zamaini haikumfanya akate tamaa katika maisha kwani aliamini ipo siku atafanikiwa.
“Mimi ni yule kijana niliyelelewa kwa umasikini wa chini kabisa, na kwetu tumezaliwa watoto saba na mimi ndiyo mtoto wa kwanza kuzaliwa kwetu , nilitoka kwetu kutafuta maisha nikiwa kijana mdogo sana na nikawa omba omba mtaani na baadaye niwa nafanya kazi za ndani kwenye majumba ya watu, lakini baadaye nikajiingiza katika biashara na nikaenda hadi nchini Uganda .” ameeleza Muchoma
Nyumba ya Muchoma
Kuhusu mafanikio aliyonayo kwa sasa ikiwemo kununua nyumba ya
kifahari ya milioni 45 za Rwanda maeno ya Kisenyi nchini humo , Muchoma
ameeleza hizo ni moja ya ndoto yake kwani alijitahidi kujinfunza vitu
vingi iliasife masikini.
“Mafanikio yakazidi na hatimaye nikapata pesa zangu nyingi na nikaenda Marekani, baade nikareje nyumbani (Rwanda) nikawa naendelea na masuala ya biashara na huko ndiko nilipopata pesa za kuweza kujenga nyumba hiyo ya kifahari.”
Lengo la kulezea historia yangu hiyo ni kuwapa moyo vijana wasikate tamaa katika maisha na kuijiona hawezei kubadirisha mambo amesema Muchoma.
COMMENTS