BOT Imeyafungia Maduka 86 Kwa Kushindwa Kutimiza Masharti

Benki kuu ya Tanzania imeyafungia maduka 86 ya kubadilishia fedha za kigeni baada ya kushindwa kutimiza masharti ikiwemo kutoa vielelezo...


Benki kuu ya Tanzania imeyafungia maduka 86 ya kubadilishia fedha za kigeni baada ya kushindwa kutimiza masharti ikiwemo kutoa vielelezo vinavyoonyesha fedha za kigeni zinazotumika kwenye biashara hiyo zimetokana na chanzo kipi.

Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya kuandika habari za kiuchmi mkoani Mtwara meneja wa kitengo kinachosimamia fedha za kigeni kutoka benki kuu ya Tanzania Eliyamringi Mandari amesema kufungwa kwa maduka hayo kunatokana na oparesheni inayoendelea nchi nzima kwa sasa yenye lengo la kuleta ufanisi wa kazi katika maduka hayo.

Amesema upareresheni hiyo inakwenda sambamba na usajili upya wa maduka hayo ya kubadilisha fedha za kigeni ambayo imetokana na kanuni mpya ya kusimamia maduka hayo lengo hasa ni kuongeza ufanisi na  mitaji katika kuendesha biashara hiyo.

Hata hivyo amesema katika oparasheni hiyo maduka 297 yametuma maombi yao huku maduka  sitini na tano yanaendelea kufanyiwa kazi, sabini na moja tayari yamepatiwa leseni mpya pamoja na matawi yake arobaini.

Amesema maduka 86 yamefutiwa leseni kutokana na kushindwa kutimiza masharti ikiwemo kueleza vyanzo vya mitaji inayotumika katika kuendesha.

Biashara hiyo na kusisitiza wiki mbili zijazo zoezi hilo litakamilika na taarifa kamili itatolewa.

Kufuatia opareheni hiyo mandari amesema ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kuendesha biashara ya fedha za kigeni bila leseni ya benki kuu adhabu yake ni faini shilingi milioni nne, ama kifungo cha miaka kumi na nne gerezani, ama vyote viwili.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: BOT Imeyafungia Maduka 86 Kwa Kushindwa Kutimiza Masharti
BOT Imeyafungia Maduka 86 Kwa Kushindwa Kutimiza Masharti
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjh3obtSvi62Bnzow7SB6a7nvmm2RFqSby6WHqKbhhFY2OEQSTX7rQ9d_CTO3UWFy65woZIoDoPR1m8r8y-j9h-jDN5OQnB390z3beqwLEI7BLxRKPnF_JZpLYND39O-2EP7t0wABfQYa8p/s640/BOT-1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjh3obtSvi62Bnzow7SB6a7nvmm2RFqSby6WHqKbhhFY2OEQSTX7rQ9d_CTO3UWFy65woZIoDoPR1m8r8y-j9h-jDN5OQnB390z3beqwLEI7BLxRKPnF_JZpLYND39O-2EP7t0wABfQYa8p/s72-c/BOT-1.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/bot-imeyafungia-maduka-86-kwa-kushindwa.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/bot-imeyafungia-maduka-86-kwa-kushindwa.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy