Mkuu wa wilaya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa Kata ya Didia Shinyanga na kuivunja kamati ya maji kutokana na kuf...
Mkuu wa wilaya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa Kata ya Didia Shinyanga na kuivunja kamati ya maji kutokana na kufanya ubadhirifu wa fedha na kukwamisha mradi huo kutofanya kazi tena
Wananchi wa kata ya Didia wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya maji iliyovunjwa kata ya Didia Selemani Msabaha akizungumza mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na wananchi na kukiri mradi huo wa maji Didia kuwa umeshidwa kuendelea kutoa huduma mara baada ya fedha za matengenezo Shilingi milioni 3.7 kukosekana
Mkaguzi wa ndani wa halmashuri ya Shinyanga vijijini Sumbukeni Malela ,akieleza jinsi ubadhirifu wa fedha ulivyotumika kwenye mradi huo wa maji Didia
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameivunja Kamati ya maji ya
kata ya Didia iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
kutokana na kufanya ubadhirifu kwenye mradi wa maji wa kisima kirefu.
Kamati hiyo inadaiwa kutafuna pesa za mradi ulioanza kujengwa mwaka
2013/2014 na kukabidhiwa mwaka 2016 na kugharimu shilingi milioni 400.16
umeshindwa kuendelea kuhudumia wananchi mara baada ya kifaa kimoja
kuharibika na kukosekana pesa za matengezo na kuufanya mradi kutaka
kufa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Didia jana
Februari 8,2018 mkuu wa wilaya aliamua kuvunja kamati hiyo na kuagiza
wajumbe wa kamati hiyo wakamatwe.
“Kamati hii kuanzia sasa nimeivunja na ninaagiza jeshi la jadi
Sungusungu watu hawa watafutwe wakamate na wapelekwe Polisi sababu ni
wahujumu uchumi na kisha wapewe muda wa kizirudisha pesa zote
walizozitafuna kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria,” alisema Matiro.
Hata hivyo mara baada ya kuivunja kamati hiyo ya maji, alisimamia zoezi
la wananchi kuchagua viongozi wengine sita wa mpito kupitia mkutano huo
wa hadhara kwa kuchaguliwa na wananchi wakiongozwa na mwenyekiti wake
Katunge Njile, huku akiagiza viongozi wote wa vitongoji kuitisha
mikutano ya hadhara na kuchagua wajumbe wawili wawili ambao wataunda
kamati ya maji ya kudumu.
Pia aliagiza kila kaya kwenye kata hiyo ya Didia yenye wakazi 4112
wachange shilingi 3000, fedha ambazo zitasaidia kununua kifaa kwenye
mradi huo wa maji chenye gharama ya shilingi milioni 3.7, ili uanze
kufanya kazi na kuondoa adha ya wananchi kutumia maji machafu sambamba
na kumtua ndoo kichwani mwanamke.
Naye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya maji Selemani Msabaha,
alikiri kuwa walishindwa kuendesha mradi huo mara baada ya pesa
kukosekana ambapo mpaka sasa kwenye akaunti kuna shilingi 129,000.
Kwa mujibu wa mkaguzi wa ndani wa halmashauri hiyo Sumbukeni Malela
kamati hiyo ilikuwa ikikusanya hadi shilingi milioni 17 na walikuwa
hawafanyi vikao na hakuna listi za manunuzi ya vifaa vinapoharibika na
kwamba kiasi cha shilingi 984,600 hazijulikani zilipo.
COMMENTS