Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua kikao cha Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSA) halmashauri ya...
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua kikao cha Umoja wa
Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSA) halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga (Vijijini) .Kushoto ni mwenyekiti wa TAHOSA wa halmashauri
hiyo Leonard Laurent. Kulia ni Kaimu mkurugezi wa halmashauri hiyo
Stewart Makali.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine MatiroMatiro
amewatahadharisha wakuu wa shule za sekondari wilayani humo kutothubutu
kuchangisha pesa kwa wazazi na wanafunzi kwa ajili ya mitihani ya shule
na shule kwani ni kwenda kinyume cha agizo la rais John Pombe Magufuli
linalokataza michango shuleni.
Matiro ametoa tahadhari hiyo leo Jumatano Februari 7,2018katika kikao cha kwanza kwa mwaka 2018 cha Umoja wa wakuu wa shule za sekondari Tanzania (TAHOSA) halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kilichofanyika katika ukumbi wa Mwalimu House Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wakuu wa shule 27 za sekondari zilizopo katika halmashauri hiyo.
Aidha aliwataka wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kutumia mapato ya ndani na juhudi za wafadhili au wadau wa elimu kufanikisha mitihani ya wilaya badala ya kuchangisha wazazi na wanafunzi.
Matiro ametoa tahadhari hiyo leo Jumatano Februari 7,2018katika kikao cha kwanza kwa mwaka 2018 cha Umoja wa wakuu wa shule za sekondari Tanzania (TAHOSA) halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kilichofanyika katika ukumbi wa Mwalimu House Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wakuu wa shule 27 za sekondari zilizopo katika halmashauri hiyo.
Aidha aliwataka wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kutumia mapato ya ndani na juhudi za wafadhili au wadau wa elimu kufanikisha mitihani ya wilaya badala ya kuchangisha wazazi na wanafunzi.
"Naomba mitihani mnayofanya ya Interschool Examination isihusishe michango yoyote kutoka kwa wazazi na wanafunzi, tukihusisha michango tunakuwa tumekwenda kinyume na kanuni, taratibu na matamko yanayotolewa na viongozi wetu”,alisisitiza .
"Hakikisheni
pia pesa za serikali zinatumika kulingana na kanuni na utaratibu
uliopangwa,zisipotumika vizuri maana yake mmeshindwa kufanya kazi
mtawajibishwa”,alieleza.
Mkuu huyo wa wilaya aliwakumbusha kuwa wakuu wa shule ndiyo wasimamizi wakuu wa shule na mambo yanapoharibika wao ndiyo watakuwa wa kwanza kuchukuliwa hatua.
“Kwa
mwongozo uliopo sasa mkuu wa shule ndiye mdhibiti ubora wa shule wa
kwanza, yaani ubora wa shule unakutegemea wewe, ina maana shule yako
ikiwa na matatizo msababishi ni wewe na mwalimu mwandamizi wa taaluma,
tumieni vizuri vitabu vya mwongozo mlivyopewa, kiongozi cha mwalimu mkuu
ili kujikita katika mazingira salama mnapotekeleza majukumu yenu", alisema Matiro.
Mkuu huyo wa wilaya pia aliwataka wakuu hao wa shule kusimamia nidhamu kwa walimu na wanafunzi na kudhibiti utoro shuleni.
Matiro
aliwataka walimu kujituma katika kazi na kuzitaka mamlaka zinazohusika
kuwachukulia hatua walimu ambao shule zao kila mara zimekuwa zikifanya
vibaya katika matokeo ya mitihani.
“Mwalimu
upo pale kila mwaka wanafunzi wanafeli, wanapata ziro, shule inakuwa ya
mwisho halafu mnamuacha tu huyo mwalimu kwanini? tuna walimu wengine
pelekeni wakajaribu Labda kuna tatizo linalosababisha hayo maana kuna
mtu mwingine kapewa majukumu yanayomzidi uwezo, mwekeni pembeni aingie
mwingine tuone mabadiliko”,aliongeza.
Matiro
aliwakumbusha pia wakuu wa shule kuwajengea wanafunzi hulka ya kupenda
michezo na kuwapatia elimu ya kujitegemea badala ya kuwapa elimu ya
darasani pekee na
Kwa
upande wake mwenyekiti wa wakuu wa shule za sekondari halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga Leonard Laurent alisema pamoja na nia njema ya rais
Magufuli kuzuia michango shuleni,jamii imelipokea agizo hilo tofauti
ambapo wazazi na jamii kwa ujumla hawajishughulishi na chochote katika
maendeleo ya shule.
“Jamii
sasa haijishughulishi na chochote,hata pale walipokuwa wameshaazimia
wao wenyewe kuchangia gharama za samani (viti na meza),chakula na miundo
mbinu kupitia kamati walizounda wenyewe hawashiriki tena”,alieleza.
Aidha
aliwaomba viongozi wa serikali kuzunguka kila kata ili kukutana
viongozi wa kata na wenyeviti wa serikali za vijiji ili watoe fasiri
sahihi juuu ya nafasi ya ushiriki wa jamii katika kuleta maendeleo ya
shule zao.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua kikao cha wakuu wa
shule za sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo
Jumatano. Aliwasisitiza kutumia pesa zinazotolewa na serikali kama
inavyotakiwa.
Wakuu wa shule za sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Matiro
aliwasisitiza wakuu hao wa shule kuwachukulia hatua watu wanaowapa
mimba wanafunzi na kuhakikisha wanatoa elimu kuhusu madhara ya ndoa na
mimba za utotoni.
Matiro pia aliagiza shule kutunza mazingira kwa kupanda miti na maua sambamba na kuimarisha usafi kwa walimu na wanafunzi
Kikao kinaendelea
Mwenyekiti
wa wakuu wa shule za sekondari halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Leonard Laurent akisoma risala kwa mgeni rasmi katika kikao hicho, Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Stewart Makali ambaye ni afisa elimu sekondari wa halmashauri hiyo akizungumza katika kikao hicho. Alisema halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu wa viti na meza 3000 katika shule za sekondari.
Katibu wa Chama cha Walimu wilaya ya Shinyanga Victoria Laurent akizungumza kwenye kikao hicho na kuwataka walimu hao wakuu kuhakikisha wanajenga vyumba vya kujistiri kwa wanafunzi wa kike.
Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Shinyanga Francis Mbonea akizungumza kwenye kikao hicho na kuwataka walimu wakuu kujituma kufanya kazi kwa bidii na kuondoa matokeo yenye sifuri shuleni kwao ili kuonyesha hamasa kwa serikali na hatimaye kushughulikia matatizo yao ikiwemo kuwalipa madeni na kuwapandisha madaraja
COMMENTS