Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi aliyekuw...
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto)
akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi aliyekuwa
akimunesha mpaka wa kijiji hicho na Pori la Akiba Mkungunero wakati wa
ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilaya ya Kondoa Mkoani
Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori
hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema
Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa
pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la
Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.
Ashatu Kijaji.
Na Hamza Temba - Kondoa, Dodoma
.....................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla jana tarehe 7
februari, 2018 ametembelea Pori la Akiba Mkungunero katika Wilaya ya
Kondoa Mkoani Dodoma na kuwataka wananchi wanaozunguka pori hilo
kusubiri uamuzi wa Serikali utakaoshirikisha Wizara yake, Wizara ya
Ardhi na Tamisemi katika kujibu maombi yao ya kutaka kupewa sehemu ya
ardhi katika pori hilo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kibinadamu.
Dk. Kigwangalla ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji na
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, alitembelea
vijiji vinne vya Ikengwa, Keikei Tangini, Keikei na Kisondoko na kufanya
mikutano ya hadhara kwa ajili ya kujiridhisha na kujifunza juu ya
mgogoro uliopo baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba Mkungunero.
"Nimefika hapa leo kujifunza juu ya mgogoro huu, nimejionea hali halisi
lakini pia nina maelezo ya wataalamu ambayo yapo kwenye maandishi naomba
niende nikayasome, niyatafakari ili niweze kushauriana na wenzangu na
mwisho wa siku tuweze kuja na suluhu ya namna ya kuondokana na
changamoto ambazo zimekuwepo.
"Niwaombe sana wakati Serikali inaendelea kutafuta suluhu ya mgogoro huu
ni vema tukafuata sheria zilizopo, tuzingatie mipaka iliyowekwa ili
tusiingie kwenye migogoro, lakini kwa sasa siwezi kwa namna yeyote ile
kutamka neno la kujibu maombi ya mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji na
wananchi yaliyotolewa hapa leo.
"Kama Serikali tutakaa, Wizara yangu, Wizara ya Ardhi na Tamisemi ili
tujue kiini cha mgogoro huu tufanye uamuzi kuwa ni maeneo gani yaongezwe
katika hifadhi kwa ajili ya wananchi au ni vitongoji vipi vifutwe,
tutaleta majibu, na jambo hili tutalifanya kwa uadilifu mkubwa bila
kumuonea mtu ili kumaliza mgogoro huu," alisisitiza Dk. Kigwangalla.
Awali akimkaribisha Waziri huyo kuzungumza na wananchi wa kijiji cha
Ikengwa, Mbunge wa jimbo hilo, Dk. Ashatu Kijaji alisema kutokana na
ukweli kuwa Serikali ya awamu ya tano inasikiliza kero za wananchi na
kuzipatia ufumbuzi, ni vema Waziri huyo akatumia hekima na kuangalia
uwezekano wa kuwapa wananchi hao Kilomita 12 za mraba kutoka kwenye
hifadhi hiyo kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kibinadamu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi
alisema mgogoro baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba Mkungunero ulinza
mwaka 2006 kufuatia zoezi la kuanzishwa kwake pamoja na lile na
uwekagi wa vigingi vya mpaka na vijiji jirani kutoshirikisha wananchi
na viongozi wa halmashauri za vijiji hoja ambayo ilipigwa na Meneja wa
Pori hilo, Emannuel Bilaso.
Aidha alisema wananchi wa vijiji hivyo wanakabiliwa na uhaba wa maeneo
ya kilimo na ufugaji, hivyo akamuomba Waziri huyo pamoja na Serikali kwa
ujumla kutumia busara kuwamegea wananchi wa vijiji hivyo eneo la
Kilomita 12 za mraba kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.
Naye Meneja wa Pori hilo, Emannuel Bilaso alisema Pori la Akiba
Mkungunero lilianzishwa kwa tangazo la Serikali Na. 307 la mwaka 1996
baada ya kupandishwa hadhi kutoka Pori Tengefu. Alisema mchakato wa
kupandisha hadhi pori hilo ulishirikisha wananchi na viongozi wa vijiji
na wilaya ambapo mihutasari mbalimbali ilisainiwa.
Alisema pori hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazochochea
mgororo huo ikiwemo kijiji kimoja cha Kisondoko kusajiliwa kimakosa
ndani ya hifadhi hiyo pamoja na malalamiko mbalimbali ya wananchi kuwa
hawakushirikishwa kwenye uanzishwaji wa pori pamoja na madai mengine
kuwa pori hilo limeingilia mipaka ya vijiji hivyo.
Pori la Akiba Mkungunero ambalo lina ukubwa wa Kilimita za Mraba 557.9
lina umuhimu mkubwa kiuchumi na kiikolojia kwa kuwa ni chanzo muhimu cha
mto Tarangire ambao ni uhai wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire na
ikolojia nzima ya ziwa Manyara. Pori hilo pia ni sehemu ya mapito na
mazalia ya wanyamapori pamoja na makazi ya wanyamapori adimu duniani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na
wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kondoa muda mfupi
baada ya kuwasili wilayana humo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa ramani
ya Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kondoa, Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika
pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini
changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili
kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa
kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta
suluhu ya mgogoro huo.
Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka
ya Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kondoa,
Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika
pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini
changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili
kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa
kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta
suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia)
akiteja jambo na Meneja wa Pori la Akiba Mkungunero, Emannuel Bilaso
wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa
Mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia)
akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi
wakati wa ziara yake ya kikazi jana katika Pori la Akiba Mkungunero
Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za
mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia
ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara
ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisondoko wilayani Kondoa jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Mkungunero na mmoja wa wahifadhi wa Pori hilo wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
COMMENTS