Huduma Serikali Ya Marekani Zakwama Tena

HUDUMA za serikali ya Marekani zimekwama baada ya bunge la Congress kushindwa kupitisha mkakati muhimu wa bajeti yake kwa wakati unaof...


HUDUMA za serikali ya Marekani zimekwama baada ya bunge la Congress kushindwa kupitisha mkakati muhimu wa bajeti yake kwa wakati unaofaa.
Wabunge walitumai kwamba watapitisha matumizi mapya kabla ya muda wa kufadhili bajeti hiyo kukamilika.

Lakini seneta wa Republican, Rand Paul, alimaliza matumaini ya kupigwa kwa kura ya haraka wakati alipoitisha mjadala bungeni kuhusu marekebisho ya matumizi.
Mnamo mwezi Januari kisa kama hicho cha kushindwa kupitisha matumizi ya serikali katika wakati unaofaa kilisababisha serikali kuwa na mkwamo wa siku tatu.
Hata hivyo, wafanyikazi wa serikali wameombwa kutumia maajenti wa nyumbani ili kupata mwelekeo kuhusu ni lini watarudi kazini.

Mabunge yote ya seneti na lile la uwakilishi ni sharti yaidhinishe matumizi hayo ya miaka miwili.
Mkwamo huo ulitarajiwa ikiwa imesalia saa moja kabla ya muda kukamilika wakati bunge la seneti lilipopiga kura ya mapumziko.
Lakini licha ya kucheleweshwa, bunge hilo linatarajiwa kupigia kura matumizi hayo.
Bunge la uwakilishi halitapiga kura yoyote hadi pale bunge la seneti litakapoidhinisha matumizi hayo.

Haijulikani ni vipi bunge la Congress litaendelea na vile huduma za umma zitakavyoathirika.
Hatua hiyo itasababisha kupanda kwa matumizi hadi $300bn (£215bn) – kitu ambacho Seneta Paul anasisitiza hawezi kuunga mkono.
Huku ufadhili wa bajeti ya idara ya ulinzi ukionekana kuwafurahisha maafisa wa masuala ya usalama, wahafidhana wanapinga athari za deni la taifa hilo.
Seneta Paul  aliwakemea wenzake wa chama cha Republican akidai ufisadi unaendelea.

”Niligombea wadhifa huu kwa sababu nilikuwa mkosoaji mkubwa wa deni la Dola trilioni nyingi  katika utawala wa Rais Obama”

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Huduma Serikali Ya Marekani Zakwama Tena
Huduma Serikali Ya Marekani Zakwama Tena
https://1.bp.blogspot.com/-FFpbVv5gM0I/Wn2rGheVOdI/AAAAAAAABkU/yGoOMsIySp49q__8ghpK9eKQLSV_fRRjACLcBGAs/s640/yogo.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-FFpbVv5gM0I/Wn2rGheVOdI/AAAAAAAABkU/yGoOMsIySp49q__8ghpK9eKQLSV_fRRjACLcBGAs/s72-c/yogo.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/huduma-serikali-ya-marekani-zakwama-tena.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/huduma-serikali-ya-marekani-zakwama-tena.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy