Mtoto Cruise Horsburgh, wa Newcastle-Upon-Tyne, Uingereza, aliyezaliwa akiwa na jino moja. MAMA mmoja, Shannon MacAllister (17) mkaz...
Mtoto Cruise Horsburgh, wa Newcastle-Upon-Tyne, Uingereza, aliyezaliwa akiwa na jino moja.
MAMA mmoja, Shannon MacAllister (17) mkazi wa Walker, Newcastle-Upon-Tyne, Uingereza, mwezi uliopita alipigwa butwaa baada ya mtoto wake kuzaliwa na jino moja kwenye ufizi wake wa chini.
Mtoto huyo wa kiume, Cruise Horsburgh, alipofungua mdomo wake alionyesha jino hilo ambalo lilimshangaza mama yake na mkunga aliyemzalisha.
Familia
iliyojaa furaha: Cruise akiwa bibi yake mkubwa, Alice McAllister
(kushoto), babu Anthony (kulia) na bibi Kim McAllister (aliyesimama
kushoto), bibi mwingine Tania Armstrong (aliyesimama kulia) na wazazi
wake Shannon McAllister na Dean Horsburgh (katikati).
Cruise alizaliwa Hospitali ya Royal Victoria ya Newcastle, Januari 27 mwaka huu ambapo ajabu hiyo ilielezwa na wataalam kwamba ni kitu adimu, kwani katika watoto 2,000 hadi 3,000 wanaozaliwa, ni mmoja tu anaweza kuzaliwa akiwa na hali hiyo.
“Lilikuwa ni jambo la ajabu, watu wengi walikuja kumwona mtoto na kushangaa, kwani wengi wao walikuwa hawajaona kitu hicho,” alisema Shannon akielezea tukio hilo ambapo kwa kawaida watoto huanza kuota meno baada ya miezi sita, japokuwa wengine huanza wakiwa hata na miezi minne.
COMMENTS