Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiongea na baadhi ya viongozi ,walimu na wanafunzi wa shule y...
Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo
Judith Laizer akiongea na baadhi ya viongozi ,walimu na wanafunzi wa
shule ya msingi Isoliwaya wakatika wa kukabidhi msaada huo kwa ajili ya
kujengea vyoo ya walimu wa shule hiyo
Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo
Judith Laizer akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa chama hicho
Leah Moto na Nancy Nyalusi walikuwa kwenye ziara ya kusherekea miaka 41
ya chama cha mapinduzi
Hili ni moja ya jengo lashule ya msingi Ilula iliyopo katika tarafa ya mazombe wilayani kilolo mkoani Iringa
WALIMU wa shule ya msingi Ilula na Isoliwaya zilizoko katika kata
ya Ilula Wilaya ya Kilolo wanakabiriwa na magonjwa ya Mlipuko kwa
kukabiliwa na changomoto ya choo.
Shule hizo zilizotenganishwa baada idadi kubwa ya wanafunzi, walimu
49 wanalazimika kutumia choo Chenye matundu mawili hali inayohatarisha
usalama wa afya zao.
Akizungumza mbele ya Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT)
wilaya ya Kilolo Judith Laizer, mwalimu Msaidizi wa shule ya Msingi
Isoliwaya, Huruma Mbena alisema hali hiyo inahatarisha afya za walimu
kutokana na changamoto hiyo.
Mbena alisema kuwa baada ya shule hizo kutenganishwa vyoo vya
walimu vilibaki kwa shule ya Ilula hivyo kutokana na idadi kubwa ya
walimu wanalazimika kutumia vyoo hivyo licha ya kutotosheleza kutokana
na idadi kubwa ya walimu.
Aidha alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya nyumba
za walimu ambao hadi sasa walimu 21 wanaishi katika nyumba za kupanga
hali inayowaletea ugumu wa maisha zaidi.Alisema kuwa changamoto nyingine
wanayokabiliana nayo ni ukosefu wa ofisi za walimu na ofisi ya mwalimu
mkuu na kulazimika kutumia moja ya darasa kama ofisi na kupunguza idadi
ya madarasa.
Akijibia hoja zilizopo kwenye risala Katibu wa umoja wa wanawake wa
Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer alisema kuwa umoja huo
umewaleta mifuko ya saruji kumi na tano (15) na bati saba kwa ajili ya
kusaidia kujenga vyoo vya walimu ili kupunguza adhabu wanayoipata.
“Kweli ukikosa huduma ya choo bora walimu hawezi kuwa huru
kufundisha wanafunzi maana anaenda chooni huku akijua kuwa wanafunzi
wake wanamtazama kwa mtazamo tofauti na ukizingatia maisha ambayo
wanaishi majumbani kwao” alisema Laizer
Laizer alisema kuwa changamoto nyingine kama ukosefu wa nyumba za
walimu,upungufu wa vyumba nane vya madarasa na ukosefu wa ofisi ya
walimu atazifikisha kwa viongozi wa wilaya na kwa mbunge wa jimbo hilo
Vennace Mwamoto.
“Hizi changamoto zenu zinatatulika kwa kuzingatia kuwa vingozi wa
wilaya hii ni wachapakazi na waadilifu kuwatumikia wananchi nauhakika
kuwa watakuja hapa na kuzitafutia ufumbuzi hizi changamoto kwa kuwa
nitazifikisha kama nilivyozichukua hapa” akisema Laizer
Lakini Laizer aliwataka viongozi wa bodi ya shule hilyo kuhakikisha
kuwa wanafanya kazi kwa ukaribu na wazazi wa shule hiyo kwa kuhakikisha
wanaanza ujenzi wa nyumba za walimu pamoja na kujenga vyumba vya
madarasa na mwishoni mbunge na halmshauri watamalizia sehemu iliyobaki.
“Naombeni nyie viongozi kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi hao
bila kuwashirikisha walimu kwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dr John Pombe Magufuli kama alivyoagiza kuwa elimu bure bila
malipo” alisema Laizer
Laizer aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kufanya kazi kubwa ya
kufaulisha kwa wastani unaolidhisha na kuwaomba kuongeza bidii
kufundisha huku wakibuni mbinu mpya za ufundishaji.
COMMENTS