Kesi Ya PEDESHEE NDAMA TOTO YA NG'OMBE Yasubiri Nyaraka Kutoka AUSTRALIA

Upande wa Mashtaka katika kesi ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu inayomkabili mfanyabiashara, Ndama Hussein maaru...


Upande wa Mashtaka katika kesi ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu inayomkabili mfanyabiashara, Ndama Hussein maarufu Pedeshee Ndama mtoto ya Ng'ombe, umeieleza mahakama kuwa wanasubiri nyaraka kutoka nchini Australia.

Ndama anakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi na kujipatia dola 540,000 za Marekani kwa njia ya udanganyifu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali, Estazia Wilson amedai leo Februari 12, 2018 mbele ya hakimu mkazi mkuu wa Mahakama hiyo, Victoria Nongwa, kuwa wameshapeleka maombi kwa ajili ya kupata nyaraka hizo.

Pia, wakili Wilson amedai kuwa mshtakiwa ni mgonjwa na leo ameshindwa kufika mahakamani hapo.

"Mheshimiwa hakimu, tunasubiri nyaraka kutoka nchini Australia na mshtakiwa leo hajafika mahakamani kwa sababu ni mgonjwa, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajaa,” amedai.

Januari 10, 2018 kesi hiyo iliahirishwa baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama hiyo kuwa wanasubiri nyaraka kutoka nchini Australia.

Kuhusu nyaraka, wakili Wilson amedai kuwa wanazosubiri ni zile walizoomba kutoka nchini Australia.

Hakimu Nongwa alikubaliana na ombi la upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 28, 2018 itakapotajwa na dhamana ya mshtakiwa inaendelea.

Ndama anakabiliwa na mashtaka matano ambayo katika shtaka la kwanza, anadaiwa kuwa Februari 20, 2014 Dar es Salaam, alighushi kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonyesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu yenye kilo 207 yenye thamani ya Dola 8,280,000 za Marekani kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.

Pia anadaiwa Machi 6, 2014, Dar es Salaam, alighushi kwa kutengeneza hati ya kibali ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam akijaribu kuonyesha kilo 207 za dhahabu kutoka nchini Congo zinatarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua si kweli.

Katika shtaka la tatu, Ndama anadaiwa Februari 20, 2014, alighushi fomu ya forodha yenye namba za usajili R.28092 akionyesha kampuni ya Muru imeilipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) dola 331,200 za Marekani kama kodi ya uingizaji wa bidhaa ambazo zina uzito wa kilo 207 za dhahabu zenye thamani ya dola 8,280,000 za Marekani kutoka Congo.

Pia, anadaiwa kuwa Februari 20, 2014 alighushi nyaraka ya bima kutoka Phoenix of Tanzania Assurance Company Ltd akionyesha kampuni ya Muru imeyawekea bima maboksi manne yaliyokuwa na dhahabu hizo.

Anadaiwa kati ya Februari 26 na Machi 3, 2014, Dar es Salaam kwa njia ya udanganyifu alijipatia kutoka kwa kampuni ya nchini Australia ya Trade TJL DTYL Limited dola 540,000 za Marekani baada ya kudanganya atawapa na kusafirisha dhahabu hizo.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Kesi Ya PEDESHEE NDAMA TOTO YA NG'OMBE Yasubiri Nyaraka Kutoka AUSTRALIA
Kesi Ya PEDESHEE NDAMA TOTO YA NG'OMBE Yasubiri Nyaraka Kutoka AUSTRALIA
https://3.bp.blogspot.com/-izOpX7kRfXw/WoKjbGgeJsI/AAAAAAAACKs/GBGp6O0M0KEBZbZYfPD_iR0rXNPV8Z-IACLcBGAs/s640/ndama.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-izOpX7kRfXw/WoKjbGgeJsI/AAAAAAAACKs/GBGp6O0M0KEBZbZYfPD_iR0rXNPV8Z-IACLcBGAs/s72-c/ndama.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/kesi-ya-pedeshee-ndama-toto-ya-ngombe.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/kesi-ya-pedeshee-ndama-toto-ya-ngombe.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy