Hizi ni dalili mbalimbali zinazojitokeza kwenye miili yetu. Japo zinaweza zisiashirie tatizo, lakini kama ikitokea zinajirudia mara kw...
Hizi
ni dalili mbalimbali zinazojitokeza kwenye miili yetu. Japo zinaweza
zisiashirie tatizo, lakini kama ikitokea zinajirudia mara kwa mara ni
vyema kupata vipimo na ushauri wa kiafya.
Dalili ya kwanza ni udhaifu wa kwenye miguu na mikono kunakoambatana na ganzi.
Ikiwa
sehemu za mikono na miguu zinadhoofika, zinakosa nguvu na kupata ganzi
na hasa dalili hizi zikitokea hadi usoni, inaweza kuwa ni dalili ya
kiharusi na hasa kama hali hii inatokea upande mmoja tu wa mwili.
Sambamba
na dalili hizi, kiharusi pia huambatana na dalili kama vile unakosa
`balansi’ wakati wa kutembea, unapata kizungunzungu na kushindwa
kutembea vizuri.
Nikukumbushe
tu msomaji, kiharusi ni ugonjwa unaosababishwa na matatizo ya
usambazwaji wa damu kwenye ubongo kutokana na kuziba au kupasuka kwa
mirija inayosambaza damu kwenye ubongo na kusababisha chembechembe za
damu kufa.
Kiharusi kwa kitaalamu kinaitwa stroke na ni maarufu kwa jina hili. Kiharusi ni moja ya magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo vya ghafla kwa miaka ya hivi karibuni.
Hivyo
pata msaada wa kitabibu haraka ikitokea unapatwa na dalili hizi pamoja
na dalili zingine kama kutoona vizuri, maumivu makali ya kichwa, kuhisi
kuchanganyikiwa au kupata shida katika kuongea.
Dalili
nyingine ni maumivu ya kifua. Maumivu ya kifua na hasa yanayoambatana
na joto kali na kutokwa na jasho, upumuaji wa shida na hata
kichefuchefu, yanapaswa kutafutiwa ufumbuzi wa kitabibu haraka.
Maumivu
ya kifua yanayodumu kwa muda mrefu yanaweza kuwa ni ishara ya magonjwa
ya moyo au shambulio la moyo na hasa kama yakitokea wakati wa kufanya
mazoezi au hata shughuli yeyote inayofanya mwili utumike.
Lakini
pia maumivu ya mara kwa mara ya kifua yanaweza kuashiria tatizo lingine
tofauti na moyo,kama vile kuganda kwa damu kwenye mapafu au mzunguko
wa damu kutokuwa sawa kwenye mapafu.
Pamoja na hayo, ni vyema kumuona daktari haraka endapo kifua kinabana na hali hii ikiwa ni ya kujirudia rudia.
Lakini
dalili nyingine ni mkojo unaoambatana na damu. Yapo matatizo mengi
ambayo yamezoeleka yanayoweza kusababisha kutoa mkojo uliochanganyika na
damu, kama vile mambukizi ya kwenye njia za mkojo na hata maambukizi ya
baadhi ya magonjwa ya zinaa ikiwa yamedumu kwa muda mrefu bila tiba.
Lakini
pia ikiwa unatoa mkojo uliochanganyika na damu, na hasa ukiambatana na
maumivu ya mgongo au hata maumivu ya chini ya kitovu, hii ni ishara
tosha kuwa unashambuliwa na baadhi ya maradhi ya figo na hasa uwepo mawe
madogo madogo kwenye figo ambao kitaalamu tunaita kidney stones.
Tatizo
hili hutokea wakati ambapo aina hii mawe yanajitengeneza na
kujikusanaya kwenye figo baada mkojo kuchujwa na yale mabaki ya mkojo
kutengeza mawe haya yatokanayo na ile chumvi chumvi.
Mawe
haya hulazimika kutoka kupitia njia inayotumika na mkojo kutoka kwenye
figo ndani hadi kwenye njia ya mkojo ya nje iliyoambatana na via vya
uzazi.
Hivyo
kupitia mchakato huu, wakati wingine mawe haya huchumbua njia ya mkojo
wakati yakiwa yanalazimika kutoka nje na kusababisha majeraha madogo
madogo kwenye njia ya mkojo na kutokwa na damu.
Ni vyema kumuona daktari ili kuangalia uwepo wa aina hii yam awe kwenye figo.
Lakini
tatizo lingine kubwa, mkojo uliochanganyika na damu mara nyingi
huashiria saratani ya kibofu, na hasa ikitokea huambatana na maumivu
yoyote hivyo ni vyema kuwahi kupata vipimo ili kuliwahi tatizo hili
katika hatua zake za awali.
COMMENTS