LIPULI FC 0-2 YANGA , Kutoka Uwanja SAMORA , IRINGA

MPIRA UMEMALIZIKA KADI Dk 90+3, Gadiel analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda akiwa amekusudia DAKIKA 5 ZA NYONGEZA Dk 90 sasa,...


MPIRA UMEMALIZIKA
KADI Dk 90+3, Gadiel analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda akiwa amekusudia
DAKIKA 5 ZA NYONGEZA

Dk 90 sasa, ni miujiza tu itaifanya Lipuli kusawazisha mabao kwa kuwa hawana mipango madhubuti kuhakikisha wanasawazisha

SUB Dk 86, Juma Mahadhi anaingia nafasi ya Raphael anayekwenda benchi
Dk 83 Chirwa tena anaingia vizuri, krosi yake inazuiliwa na kuwa kona, inachongwa na kuokolewa, unakuwa wa kurushwa

SUB Dk 81, Mwashiuya anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Maka Edward
Dk 80 sasa, kipa Kabwili wa Yanga yuko chini baada ya kugongana na Salamba, anapatiwa matibabu
Dk 73 Busungu anamtoka Kessy na kupiga krosi safi kabisa, lakini Zawadi anaruka legevu na kuupiga juu ya lango, goal kick

SUB Dk 71 Zawadi MAwia anaingia upande wa Lipuli, Mussa Nampaka anakwenda kupumzika
Dk 70 sasa, hakuna matumaini kwamba Lipuli watasawazisha kwa kuwa hawana mipango bora
Dk 59 Yondani yuko chini anatibiwa baada ya kugongwa na mpira

Dk 58, Lipuli wanalisakama lango la Yanga, wanapata kona, inachongwa lakini Yanga wanaondosha
GOOOOOOOOO Dk 55, Yanga wanapiga kaunta atak ya uhakika ni Tshishimbi, Buswita, Chirwa anapiga krosi inamkuta Buswita ambaye anamchambua kipa na kuandika bao safi la pili la Yanga leo KADI Dk 54, Mwashiuya analambwa kadi ya njano kutokana na kumchezea kindava Kalihe

Dk 48, Busungu anaachia mkwaju mkali kabisa, Kabwili anapangua kwa ustadi mkubwa
Dk 47, Salamba anaachia mkwaju mkali, Kabwili anapangua vizuri lakini mwamuzi anasema ilikuwa ni offside tayari

Dk 46, Lipuli wanajaribu mara ya pili lakini bado inaonekana hawako makini
Dk 45, Lipuli wanaanza kwa kasi kabisa hapa lakini Yanga wako makini

MAPUMZIKO
DAKIKA 10 ZA NYONGEZA
Dk 45, krosi safi, Salamba anapiga kichwa vizuri lakini goal kick
Dk 42, krosi nzuri ya Chirwa, Martin anaruka na kupiga kichwa, goal kick
KADI Dk 41, Kabwili analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda kwa makusudi
Dk 42, krosi nzuri ya Chirwa, Martin anaruka na kupiga kichwa, goal kick
KADI Dk 41, Kabwili analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda kwa makusudi
Dk 40 mkwaju wa adhabu unachongwa na Salamba, lakini faulo dhaiiifuuuu, goal kick
Dk 38 sasa, Mwashiuya anafanya madhambi nje kidogo ya boksi la Yanga. Naye yuko chini, wote wanatibiwa

Dk 34, nafasi nzuri kwa Yanga lakini Raphael anaachia shuti dhaifu kabisa
Dk 30, Shambulizi kali la kwanza la Lipuli, mkwaju mkali Kabwili anaokoa lakini Mnyate anapiga shuti kuuubwa, goal kick
DK 29, Mpira ulisimama, mchezaji Lipuli akilalama kupigwa kiwikoDk 26 Martin anaachia mwaju mkali kwelikweli, Aghaton anapangua na kuwa kona, inachongwa na Kessy, Tshishimbi anapiga kichwa, goal kick

Dk 24,Kona safi inachongwa, Yanga wanaokoa inakuwa kona tena lakini Lipuli wanafanya madhambi tena na Erick Onoka, mwamuzi wa leo, anasema ni faulo
DK 22, Lipuli FC nao wanapata kona, inachongwa na Mganga, lakini imezuiwa kwa kuwa mwamuzi anazuia maana kipa Kabwili yuko chini pale

GOOOOOOOOOO Dk 19 kona safi ya Kessy, Martin anaipiga kichwa, kipa anapangua na mpira unamkuta Tshishimbi akiwa na nyavu anaachia shuti kali la makusudi na kuandika bao safi la kwanza la YangaDk 18, Chirwa anaingia vizuri, Lipuli wanatoa na kuwa kona
SUB Dk 17, Yanga wanamtoa Rostand ambaye ameshindwa kuendelea na nafasi yake inachukuliwa na kinda Ramadhani Kabwili
Dk 14 sasa, zimepita dakika 2, kipa wa Yanga yuko chini akipatiwa matibabu
Dk 10 sasa, bado hakuna mashambulizi makali sana kwa kuwa mpira zaidi uko katikati ya uwanja
DK 8, Rostand anatoka na kudaka vizuri kabisa krosi nzuri la Salamba ambaye anaonekana kuwa mwiba katika ngome ya YangaDk 6 Yanga wanaingia vizuri tena, krosi nzuri ya Gadiel lakini kipa wa Lipuli, anawahi
Dk 3, Lipuli wanaingia vizuri katika lango la Yanga lakini Jamal Mnyate anadhibitiwa vizuri
Dk 1, Mechi imeanza kwa kasi na Yanga wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Mwadui FC lakini ni goal kick.Hali ya hewa ni joto kali, si baridi kama Iringa ilivyozoeleka.

KIKOSI CHA LIPULI LEO

1. Agathon Anthon
 2. Steven Mganga
3. Ally Mtoni
4. Martin Kazila
5. Joseph Owino
 6. Novatus Lufunga
7. Seif Rashid
8. Mussa Nampaka
9. Malimi Busungu
10. Adam Salamba
11.Jamal Mnyate

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: LIPULI FC 0-2 YANGA , Kutoka Uwanja SAMORA , IRINGA
LIPULI FC 0-2 YANGA , Kutoka Uwanja SAMORA , IRINGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9UJJIr-zYcX5TSfGSo5WleFOqVpadEHZ1btizOb-hg5jOmuxrh_kn3Cc22U2BYJCFm45sOMz9NpoRqWRFa7uW96TXLp5DxJ8zjd88ynDN_Tu8hPpjsvDqAolPrzffZ3V_HNFMK-LYl_R-/s640/kikosi.PNG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9UJJIr-zYcX5TSfGSo5WleFOqVpadEHZ1btizOb-hg5jOmuxrh_kn3Cc22U2BYJCFm45sOMz9NpoRqWRFa7uW96TXLp5DxJ8zjd88ynDN_Tu8hPpjsvDqAolPrzffZ3V_HNFMK-LYl_R-/s72-c/kikosi.PNG
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/lipuli-fc-0-2-yanga-kutoka-uwanja.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/lipuli-fc-0-2-yanga-kutoka-uwanja.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy