Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa amewapongeza maaskofu kwa kuunga mkono mambo aliyosema wamek...
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa amewapongeza maaskofu kwa kuunga
mkono mambo aliyosema wamekuwa wakiyapigania.
Lowassa ametoa pongezi hizo jana
Februari 11,2018 akimnadi mgombea ubunge jimbo la Kinondoni, Salum
Mwalimu katika Kata ya Kijitonyama.
“Leo kwenye magazeti wameandika kwamba
Baraza la Maaskofu wamezungumzia mambo ambayo tumekuwa tunayasema kila
siku, kuhusu kuzuia uhuru wa kuzungumza na suala la maadili.
Ninawashukuru sana maaskofu, ninawapongeza sana kwa kuunga mkono ambayo
tumekuwa tunayasema,” amesema Lowassa.
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
(TEC), limetoa ujumbe wa Kwaresima wa mwaka 2018 ndani yake likitoa
msimamo kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini.
Lowassa akimnadi Mwalimu alisema
anamfahamu kwamba ni kijana shupavu na mchapa kazi ambaye akipewa kura
wananchi wa Kinondoni watapata maendeleo.
“Kinondoni msilale mpaka kieleweke. Mchagueni Salum Mwalimu akawaletee maendeleo,” amesema.
Mwalimu akiomba kura amesema Kinondoni ni watu ambao wanajitambua.
“Kinondoni ni watu mnaojitambua, ni watu
ambao mlijitoa mwaka 2015, wengine waliachika. Ninawapenda sana,
ninajua nina deni kubwa la kuwalipa,” amesema.
Mwalimu amesema, “Ninapozungumza najua
ninazungumza na wajanja ambao hawadanganyiki. Tangu juzi, wenzangu
wameleta fedha hapa Kijitonyama kwa ajili ya kununua shahada.”
Amesema waliposikia anagombea ubunge walipata hofu kubwa, vikao vikawa haviishi wakitafakari itakuwaje nikienda bungeni.
COMMENTS