Mahakama Yaagiza Nabii Titto Apime Upya Akili

MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imeagiza mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma Tito Machibya, maarufu kama ‘Nabii Tito’ (45) kupim...


MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imeagiza mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma Tito Machibya, maarufu kama ‘Nabii Tito’ (45) kupimwa akili upya katika Taasisi ya Afya ya Akili ya Mirembe Isanga mkoani Dodoma ili kuriridhisha kama ana matatizo ya akili.
Licha ya kuagizwa mtuhumiwa huyo kufanyiwa vipimo upya, mahakama pia imetaka kuwasilishwa kwa vielelezo kama kweli ana tatizo hilo kama alivyoieleza mahakama.
Nabii Tito anashtakiwa kwa kosa la kujaribu kujiua kwa kutumia wembe.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha, alisema jana kuwa kutokana na mshtakiwa kuieleza mahakama kuwa ana matatizo ya akili na alifanya tukio hilo kutokana na kusikia vitu ambavyo vilikuwa vinamwamuru akate, mahakama itabidi  ipate vielelezo ambavyo vitathibitisha anachokisema.

Karayemaha alisema kutokana na kifungu namba 219 (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, kama mshtakiwa atabainika kweli ana matatizo ya afya ya akili, mahakama itaamua kuwa alivyofanya tukio hilo hakuwa na akili timamu, hivyo hana hatia.

“Mshitakiwa anadai kuwa ana matatizo ya akili na amekuwa akitibiwa katika hospitali mbalimbli ikiwemo ya Maweni.  Mahakama hii inaagiza vielelezo vyake vyote viletwe hapa lakini pia apelekwe kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya ya akili Mirembe Isanga,” alisema Karayemaha.
                 
NABII TITO ALIVYOKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA
Pia alisema kama mshtakiwa atabainika kuwa hana tatizo lolote la afya ya akili kwa mujibu wa vielelezo vyake pamoja na vipimo atakavyofanyiwa, atakuwa na kesi ya kujibu.

“Kutokana na hili aliloiambia mahakama kuwa ana matatizo ya akili hata suala la dhamana tunaliweka pembeni kwanza kwa sababu hawezi kujieleza lakini kama itabainika kuwa hana matatizo ya akili kutokana na vielelezo vitakavyoletwa pamoja na vipimo vitakavyofanyika, suala la dhamana litafanyiwa kazi,”alisema.

Hata hivyo alisema mshtakiwa huyo anarudi rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa  Februari 19,  mwaka huu.
Wakati kesi itakapotajwa vielelezo vyote pamoja na vipimo vinatakiwa kuwa tayari vimeshawasilishwa mbele ya mahakama hiyo.

Nabii Tito anashtakiwa kwa tuhuma za kutaka kujiua kwa kujikata na wembe na kujijeruhi kwenye maeneo ya tumbo Januari 25, mwaka huu, katika mtaa huo wa Ng’ong’ona alipokuwa akikaguliwa na polisi.


CHANZO: NIPASHE

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Mahakama Yaagiza Nabii Titto Apime Upya Akili
Mahakama Yaagiza Nabii Titto Apime Upya Akili
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi9el48v5L0ru6wSla21vvdUyhiJzvmy5UBFbc1hvh091hFC9ey0qK_iNmKl2HYCVouXzkb564iXIJ85HbEOSrCxxqz9Dor6vIIEMW_td0adszd22D_wOJ5hqqofLimGb1R7_TCtr4_4ZZd/s640/tito-2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi9el48v5L0ru6wSla21vvdUyhiJzvmy5UBFbc1hvh091hFC9ey0qK_iNmKl2HYCVouXzkb564iXIJ85HbEOSrCxxqz9Dor6vIIEMW_td0adszd22D_wOJ5hqqofLimGb1R7_TCtr4_4ZZd/s72-c/tito-2.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/mahakama-yaagiza-nabii-titto-apime-upya.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/mahakama-yaagiza-nabii-titto-apime-upya.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy