Makamu Wa Rais Azindua Mradi Wa Kuendeleza Utalii Kanda Ya Kusini

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imedhamiria kuleta mabadiliko ya dhati katika s...


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imedhamiria kuleta mabadiliko ya dhati katika sekta ya utalii kwa kuhakikisha inatanua mtandao wa barabara na pia kuweka mikakati dhabiti ya kuviendeleza vivutio vya utalii viliovyoko kanda ya Kusini ili vichangie ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii kanda ya kusini mwa Tanzania uliofanyika Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Alisema Serikali imeendelea kuandaa na kutekeleza mipango mikakati mabali mbali kwa lengo la kuhakikisha shughuli za utalii zinasambaa nchi nzima .

Hata hivyo amasema katika kuendeleza utalii kanda ya kusini, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo mwenye masharti nafuu Dola za kimarekani milioni 150 kutoka benki ya Dunia ambapo mradi huo utatekelezwa kwa miaka 6 kuanzia 2017/2018.
Mradi huo wenye lengo kuu la kukuza utalii na kipato kwa wananchi kwa kuboresha miundo mbinu, kujenga uwezo katika usimamizi wa maliasili na kuwawezesha wananchi wanaozunguka hifadhi kuzalisha kwa tija

“Kama nilivyosema hapo awali mradi huu utajulikana kama Resilient Natural Resource for Tourism and Growth (REGROW) na utaanza kutekelezwa katika maeneo ya hifadhi ya Taifa za Ruaha, Mikumi, Udzungwa na Pori la Akiba Selous,“alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais ameiagiza Baraza la Mazingira lililokuwa chini ya Ofisi yake kuharakisha tathmini ya mazingira ya bonde la mto ruaha mkuu ili kuhakikisha kuwa mradi huu unatekelezwa kwa ufanisi bila athari zozote baadaye za mazingira.

Makamu wa Rais alielekeza taasisi zote zinazohusika zikiwemo Sekretarieti za mikoa, Halmashauri za Wilaya na Vijiji kutoa ushirikiano wa kutosha wa kufanikisha utekelezaji wa shughuli za mradi.
“Tuhakikishe sheria zinafuatwa na hakuna uvamizi wala shughuli za binadamu kwenye vyanzo vya maji na hifadhi. Wahenga wanasema tunza mazingira yako yakutunze”.
Makamu wa Rais aliwashukuru benki ya Dunia kwa kukubali kukopesha mkopo wenye masharti nafuu .


Aidha kabla ya Makamu wa Rais kuzungumza, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla alisema Sekta ya Utalii ni moja ya sekta za kipaumbele katika uchumi wa Tanzania ambapo takribani asilia 20 ya pato la Taifa linatokana na utalii na robo ya fedha za kigeni zinatokana na Utalii.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Makamu Wa Rais Azindua Mradi Wa Kuendeleza Utalii Kanda Ya Kusini
Makamu Wa Rais Azindua Mradi Wa Kuendeleza Utalii Kanda Ya Kusini
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0Fqlu0TD8s4hU-KUN4VstswB9ePfT5IipFNfgOs5YNYuYNFIwKuCSz7ZyU_eZp9-lj4w3tyswwrXH2qY4AobuWTzDTM9hXrMIT2xL76jhgSmjtGSwK1xSe11CyHLvDMg5YEQ48B0opEpf/s640/zindua.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0Fqlu0TD8s4hU-KUN4VstswB9ePfT5IipFNfgOs5YNYuYNFIwKuCSz7ZyU_eZp9-lj4w3tyswwrXH2qY4AobuWTzDTM9hXrMIT2xL76jhgSmjtGSwK1xSe11CyHLvDMg5YEQ48B0opEpf/s72-c/zindua.png
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/makamu-wa-rais-azindua-mradi-wa.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/makamu-wa-rais-azindua-mradi-wa.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy