Mwanaume mmoja nchini Uingereza amekuwa agenda katika mijadala siku za hivi karibuni baada ya kukataa kabisa kujisaidia haja kubwa na h...
Mwanaume mmoja nchini Uingereza amekuwa agenda katika mijadala siku za
hivi karibuni baada ya kukataa kabisa kujisaidia haja kubwa na hadi sasa
zikiwa zimepita siku 20, akihisiwa kuwa anatembea na dawa za kulevya
tumboni.
Polisi wanaomshikilia wameeleza kuwa wamekuwa wakimwangalia saa zote
kusubiri wakati atakaojisaidia lakini bado hajafanya hivyo, lakini hata
hivyo wameeleza kujipanga kwao kuendelea kumweka chini ya uangalizi wao
na kusubiri hadi atakapoamua kujisaidia.
Kwenye kutafuta taarifa za kidaktari kuhusu uwezekano wa mtu huyo
kuhatarisha maisha yake au la kwa kitendo hicho, Shirika la Utangazaji
la BBC Uingereza limezungumza na Trish Macnair, wa Primary Care Society
for Gastroenterology.
Trish ameeleza kuwa mwanaume huyo hatoweza kuendelea kukaa bila
kujisaidia kwa muda mrefu kama anavyofikiri kwa itafika kipindi mwili
utakataa kuendelea kutunza uchafu.
“Utafika muda atasikia tumbo lake likisogea, japokuwa anakataa kula
jambo linalofanya urahisi wa kuweza kukaa bila kwenda chooni, tumbo
litaanza kusogea tu, kwani litakuwa limejaa chakula ambacho ni uchafu.” –
Trish Macnair
COMMENTS