Hatimaye tamasha kubwa la muziki Afrika Mashariki, Sauti za Busara limefunguliwa rasmi leo katika eneo la Ngome Kongwe kisiwani Zanzibar...
Hatimaye tamasha kubwa la muziki Afrika Mashariki, Sauti za Busara limefunguliwa rasmi leo katika eneo la Ngome Kongwe kisiwani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Tamasha la Suati za Busara, Yusuf Mahmoud
Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa Tamasha hilo Yusufu Mahamoud amesema kuwa tamasha hilo limeanza rasmi leo na litadumu kwa siku nne mfululizo kwa ajili ya kuleta burudani na vionjo vya muziki kutoka sehemu tofauti duniani.
“Gearide hili ni burudani ya aina yake ambalo linakupa muongozo wa tamasha lilivyo na haupaswi mtu kukosa kwani utakuwa unakosa kuona na kufaidi uhondo wa muziki wa mataifa mbalimbali duniani waliokuja kuonyesha radha na utamaduni wao,” amesema.
Vile vile Yusuf alisisitiza kuwa “Tamasha hili sio tu kutoa burudani bali pia limekuwa likitangaza taifa letu la Tanzania pamoja na vivutio vyake.”
Licha ya chang’amoto zilizopo za wadhamini ila tamasha la Sauti za Busara limekuwa likikusanya watu kutoka mataifa mbalimbali kushuhudia muziki wenye vionjo tofauti.
COMMENTS