Ushindi wa goli moja la Tottenham dhidi ya Arsenal wiki iliyopita, linamshawishi Meneja wa timu hiyo, Mauricio Pochettino kumtaja mfun...
Ushindi
wa goli moja la Tottenham dhidi ya Arsenal wiki iliyopita,
linamshawishi Meneja wa timu hiyo, Mauricio Pochettino kumtaja mfungaji
wake, Harry Kane kuwa ni ‘jembe’ la sasa na baadaye kwa timu hiyo.
Akitumia
urefu wake, Kane aliiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa 1-0
kwenye uwanja wa Wembley dhidi ya washindani wao wa soka kaskazini mwa
jijini Londoni nchini Uingereza.
Kane
aliruka juu na kumzidi Laurent Koscielny wa Arsenal katika dakika ya 49
na kuuelekeza mpira wa krosi uliopigwa na Ben Davies, kisha kumuacha
kipa Petr Cech wa Arsenal ‘akigaagaa’ na kuandika goli hilo
lililoiwezesha Tottenham maarufu kama Spurs kupanda hadi nafasi ya Ligi
Kuu ya Uingereza.
“Harry
Kane hajapitwa na wakati, ni muhimu kwa wakati huu na ujao,’amesema
Pochettino alipolizungumzia goli safi la mchezaji huyo na kuongeza,
“tunajivuna sana kwa yeye kuwa upande wetu.”
Kabla
ya ushindi huo, Spurs ilipata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya ‘mashetani
wekundu’-Manchester United na kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool.
“Ninawapongeza
wachezaji wetu, tumekuwa na mechi kubwa tatu za mfululizo na wamecheza
kwa kiwango cha kuridhisha,” amesema Meneja huyo, raia wa Argentina.
Tottenham waliuanza mchezo dhidi ya Arsenal ‘kizembe’ na kuwafanya washindani wao kutawala mchezo.
Lakini Tottenham iliwazidi ujanja Arsenal ‘waliopotezana’ na kuruhusu matokeo ya mwisho kuwa 1-0.
COMMENTS