Mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi umezindua maktaba iliyogharimu shilingi milioni 22.4 kwenye shule ya sekondari Bugisha iliyopo kati...
Mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi
umezindua maktaba iliyogharimu shilingi milioni 22.4 kwenye shule ya
sekondari Bugisha iliyopo katika kata ya Mondo wilayani Kahama mkoani
Shinyanga kwa lengo la kusaidia wanafunzi na walimu kuchangia katika
kuboresha ubora wa elimu inayotolewa.
Maktaba hiyo imezinduliwa leo Alhamis
Februari 8,2018 na Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson
Msumba na kuhudhuriwa pia na Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na
Bulyanhulu,Benedict Busunzu.
Hii ni maktaba ya pili katika wilaya ya
Kahama kuzinduliwa na mgodi huo ambapo mwaka 2017 mgodi wa Buzwagi
ulianzisha maktaba ya jamii katika kata ya Kagongwa ili kutoa rasilimali
za elimu ya aina mbalimbali kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Akizungumza wakati uzinduzi huo, Meneja
Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu,Benedict Busunzu maktaba hiyo
itasaidia kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi kutoka jamii
inayouzunguka mgodi wa Buzwagi.
Alisema kupitia mpango wa Acacia wa
maendeleo ya jamii wameamua kushirikiana na shirika la kimataifa la Read
International kuboresha jengo moja la shule hiyo na kuliwekea samani
kwa ajili ya matumizi ya maktaba.
“Read International ni wadau wetu
wakubwa hasa katika masuala ya elimu na wamekuwa chachu ya kuleta
maendeleo,kwa kutambua umuhimu wao tuliamua kukaa chini na kuamua
kukarabati jengo moja na kulifanya maktaba ili vijana wetu wapate mahali
pa kupatia maarifa zaidi”,alieleza.
Busunzu alisema Acacia itaendelea kuunga
mkono sekta ya elimu nchini kwa njia ya kujenga miundombinu ya shule
kama vile vyumba vya madarasa,nyumba za walimu,vyoo na maabara na kutoa
misaada kwa wanafunzi kupitia vifaa vya elimu mfano vitabu,sare na ada
kupitia programu ya CanEducate.
“Misaada inayotolewa na Acacia katika
sekta ya elimu ni sehemu ya sera ya wajibikaji kwa jamii ya kampuni
inayojikita katika kuhakikisha jamii inakuwa endelevu kupitia sekta ya
elimu na sera hiyo inachangia moja kwa moja maono ya taifa hadi kufikia
mwaka 2025 na malengo ya nchi ya kuleta maendeleo endelevu kwa
kuhakikisha jamii inapata elimu iliyo bora”,alieleza.
Naye Mwakilishi wa shirika la Read
International linalojihusisha na masuala ya elimu,Esther Kalwinzi mgodi
wa Buzwagi ndiyo uliotoa shilingi milioni 22.4 kwa ajili kukarabati
darasa kuwa maktaba.
“Jumla ya vitabu 1,278 vimehifadhiwa
katika maktaba hii ambayo itahudumia wanafunzi wapatao 290 na walimu 23
na jumla ya gharama za marekebisho ya jengo hili,vitabu na samani za
maktaba ni shilingi 22,442,953”,alifafanua Kalwinzi.
Kwa upande wake,mgeni rasmi katika hafla
hiyo,Mkurugenzi wa Mji wa Kahama,Underson Msumba aliushukuru mgodi huo
kwa kuendelea kuwa karibu na jamii inayowazunguka na kushirikiana katika
shughuli za maendeleo.
“Wakati mwingine huwa nafikiria bila
mgodi Kahama ingekuwaje,kwa kweli mgodi umefanya juhudi nyingi katika
kuboresha sekta ya elimu katika wilaya yetu,ninaamini uwepo wa maktaba
hii utawafanya wanafunzi kufanya vizuri zaidi katika masomo yao”,alisema
Msumba.
Aidha aliwataka wanafunzi kuzingatia
masomo yao huku akisisitiza kuwa elimu ndiyo urithi pekee wa kudumu na
wenye kubadilisha maisha yao.
Muonekano wa jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bugisha lililoboreshwa na mgodi wa Buzwagi kwa kushirikiana na Read International
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
Kahama Mji Underson Msumba,meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na
Bulyanhulu Benedict Busunzu ,viongozi mbalimbali wa kata ya Mondo,walimu
na wanafunzi wakiwa nje ya jengo hilo la maktaba kabla ya kuzinduliwa
rasmi
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa
Kahama,Underson Msumba akikata utepe kuzindua rasmi jengo la maktaba
katika shule ya sekondari Bugisha. Katikati ni Meneja mkuu wa migodi ya
Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu.Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi
wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi akifuatiwa na diwani
wa kata ya Mondo Kija Peja
Mwakilishi wa shirika la Read
International ,Esther Kalwinzi akionesha sehemu ya kuangalia orodha/aina
ya vitabu vilivyopo katika maktaba hiyo
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson Msumba akiangalia vitabu katika maktaba ya shule ya sekondari Bugisha
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa
Kahama,Underson Msumba na Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu
Benedict Busunzu wakisoma vitabu ndani ya maktaba ya shule ya sekondari
Bugisha
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson Msumba akiangalia mandhari ya maktaba hiyo
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
Kahama Mji Underson Msumba,meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na
Bulyanhulu Benedict Busunzu ,viongozi mbalimbali wa kata ya Mondo,walimu
na wanafunzi wakiwa nje ya jengo la maktaba baada ya uzinduzi
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji Underson Msumba akiwasisitiza wanafunzi kuzingatia masomo yao
Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na
Bulyanhulu Benedict Busunzu akielezea namna walivyoshirikiana na shirika
la Read International katika kufanikisha ukarabati wa jengo hilo la
maktaba
Mwakilishi wa shirika la Read
International ,Esther Kalwinzi akizungumza wakati wa hafla fupi ya
uzinduzi wa jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bugisha
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji Underson Msumba
Mkuu wa shule ya sekondari Bugisha
Limbuzizi Magumba akiushuru mgodi wa Buzwagi kwa kutoa shilingi milioni
22.4 kwa ajili ya ukarabati wa maktaba katika shule yake
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bugisha wakiimba shairi wakati wa hafla ya kuzindua maktaba katika shule hiyo
Mwanafunzi Tedy Martine akisoma risala
akisoma risala kwa mgeni rasmi.Alizitaja miongoni mwa changamoto
zilizopo katika shule hiyo kuwa ni upungu wa viti na meza hali
inayowafanya wakae wawili wawili lakini pia upungufu wa walimu wa masomo
ya sayansi.
Diwani wa kata ya Mondo Kija Peja
akiushukuru mgodi wa Buzwagi kwa kuendelea kusaidia jamii na kuomba
ushirikiano uendelee kuwepo.
COMMENTS