Msukuma Amtolea Povu la Mwaka Waziri Wa JPM

MBUNGE na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amemshambulia kwa maneno Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina juu ya ‘opera...


MBUNGE na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amemshambulia kwa maneno Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina juu ya ‘operation’ anazozifanya za kionevu za kupambana na uvuvi haramu kwa kumwambia aache kufanya kazi kwa mihemuko.


Msukuma ameeleza hayo katika mkutano wa 10 kikao cha sita cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati akichangia uwasilishaji wa kamati ya kudumu ya Bunge ya kilimo, mifugo na maji baada ya kupita miezi kadhaa tokea Waziri Mpina kutoa kauli yake kuachia madaraka endapo tatizo la uvuvi haramu litaendelea kuwa sugu nchini jambo ambalo kwa sasa Msukuma anadai kiongozi huyo analifanya bila ya kufuata sheria zilizopo kwa kuzuia watu wasivue dagaa na kupelekea kuwapa athari wananchi wanyonge na kumuomba aundiwe tume ya uchunguzi yeye timu yake.

“Toka nazaliwa sijawahi kuona sheria hizi zinazotumiwa na Waziri wa Mifugo Mpina, umri wangu huu nimeshuhudia awamu zote za Mawaziri. Nafikilia kwamba ndio tunaanza kutunga sheria au hii ilikuwa imefichwa ndio inaibuka. Sijawahi kuona Waziri anasimama na kujisifu kwamba kwao hakuna samaki na kutamani watu wote wasile samaki. Mungu ametupa neema tofauti, sijawahi kuona mtu anaenda kukamata mitego dakika mbili faini hana unachoma nyavu zake bila ya kuhakikisha kwamba ni feki au laa”, amesema Msukuma.

Aidha, Msukuma amesema ana muhitaji Waziri huyo siku akihudhuria Bunge basi aweke wazi kuhusiana na sheria hizo anazozitumia amezitoa wapi na kama akishindwa kutokea katika kipindi basi watamsubiri katika Bunge la bajeti ili wambane vizuri juu ya hilo.

“Nitoe rai kwa Mawaziri kwamba Mawaziri wa aina kama hii nina washauri wapunguze mihemuko kwa sababu hata sisi tunatamani kuendelea kuwa Wabunge humu ndani lakini kwa ‘dizaini’ mnayoenda mtuambie mmewapanga wabunge wa kina nani ambao mnataka wawe wabunge maeneo yetu. Nina zungumza kwa wabunge wanaotoka Kanda ya Ziwa sidhani kama sisi tutarudi humu Bungeni”, amesisitiza Msukuma.


Kwa upande mwingine, Msukuma amemtaka Waziri Mpina na timu yake kiujumla wajipange kuwafundisha wavuvi na wala sio kuwafilisi.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Msukuma Amtolea Povu la Mwaka Waziri Wa JPM
Msukuma Amtolea Povu la Mwaka Waziri Wa JPM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmhOLLTUr5hH5PYP-up5mYrGvo_t-ntdNbUn_YU7uIweLgc_X2XhGVKKCf2hMWYAt_5cmXucGwy_rCZ3nUfbfcUqNwOKKeqv8Ef6oV5PqJaRnqztRv8UpFmFm8VWUFBLOy4_fpMVyadthl/s640/msukuma.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmhOLLTUr5hH5PYP-up5mYrGvo_t-ntdNbUn_YU7uIweLgc_X2XhGVKKCf2hMWYAt_5cmXucGwy_rCZ3nUfbfcUqNwOKKeqv8Ef6oV5PqJaRnqztRv8UpFmFm8VWUFBLOy4_fpMVyadthl/s72-c/msukuma.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/msukuma-amtolea-povu-la-mwaka-waziri-wa.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/msukuma-amtolea-povu-la-mwaka-waziri-wa.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy