Ni Kweri IDRIS Anateswa Na Kivuli Cha JOTI !

Idris. UNAPOTAJA waigizaji wanaofanya vizuri kwa sasa Bongo, huwezi kuacha kumzungumzia, Idris Sultan. Idris ambaye aliwahi kushi...


Idris.

UNAPOTAJA waigizaji wanaofanya vizuri kwa sasa Bongo, huwezi kuacha kumzungumzia, Idris Sultan. Idris ambaye aliwahi kushiriki kwenye Shindano la Big Brother Afrika, ni muigizaji na mchekeshaji ambaye anaonekana kuwa kwenye mafanikio makubwa kwenye ‘karia’ yake hivi sasa, kutokana na kuonesha project nyingi anazofanya, dili za matangazo pamoja na mambo mengine ya kijamii anayoshiriki.

Aina ya uchekeshaji wake wa kuingiza sauti kwenye video zinazoonesha mazungumzo ya watu maarufu, mahojiano au hotuba ni miongoni mwa vitu vinavyomfanya azungumziwe sana kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram.
Lakini mbali na hilo kiu ya watu wengi ni kutaka kufahamu staa huyo kwa sasa anatoka na nani? Showbiz Xtra imemtafuta, huyu hapa anafunguka kila kitu:

Showbiz: Vipi kuhusu kazi za vichekesho, umeonekana kuzifanya kwa namna ya tofauti kwa sasa, idea hiyo ulitoa wapi na unaona inakupeleka wapi?

Idris: Ni ubunifu tu. Unajua unapokuwa muigizaji unatakiwa kuwa mbunifu na kuangalia kitu ambacho hakipo ndiyo ufanye ili kuleta utofauti. Kiufupi naona kwa sasa watu wananielewa na bila shaka itanipeleka mbali.

Showbiz: Kwa Bongo nani unafikiri ni mshindani wako kwenye masuala ya kuchekesha?

Idris: Comedy imegawanyika kwenye makundi kadhaa, sasa kwenye upande wa comedy news na comedy fake sina mshindani. Nafanya vitu vya tofauti sana na wachekeshaji wa Kitanzania, lakini kwenye upande wa comedy skit yaani uchekeshaji wa maigizo, Joti nafikiri ni mtu ambaye nina kazi ya kumpoteza. Nakifukuza kivuli chake, naamini nitakipata tu.


Showbiz: Tuliwahi kusikia kuna muvi ambayo uliitwa kuifanya Marakeni imeishia wapi?


Joti.

Idris: Ndiyo kipindi chake. Kama unakumbuka niliwahi kuzungumza na wewe kwamba muvi hiyo iitwayo Ballin ya Hollywood, tutaanza kuishuti mwanzoni mwa mwaka huu. Sasa uzalishaji upo kwenye hatua za mwanzo na bajeti yake ni dola milioni tano za Kimarekani.

Showbiz: Unagawaje muda wako ukiwa mtangazaji, mchekeshaji na muigizaji?

Idris: Kazi zote zinategemeana na sina tatizo kabisa na muda wangu. Asubuhi nakuwa Choice FM kwenye kipindi changu, mchana na-deal na project yangu ya Foreman ambayo ni brand ya viatu na usiku nakomaa na script za movie, series na vichekesho.

Showbiz: Hivi karibuni umeonekana ukiwa bize na muigizaji kutoka Nigeria, Ramsey Noah, nini tutegemee kutoka kwenu?

Idris: Ramsey kwa sasa ni kaka na ni kama ndugu yangu. Ninashauriana naye mambo mengi sana na mtegemee kuona project za kimataifa kutoka kwetu kwa sababu mipango ipo na tupo katika hatua za kuifanyia kazi.

Showbiz: Samantha Jannsen ambaye ni muhamasishaji, mbali na video yenu ya kimahaba katika siku yake ya kuzaliwa kusambaa umekuwa ukitajwa kutoka naye kimapenzi, kuna ukweli gani katika hili?

Idris: Yule ni zaidi ya mshikaji, ila kwa sasa nisingependa kumuelezea sana.


Showbiz: Baada ya dili lako la kutangaza nguo za ndani, ulitukanwa sana mitandaoni baada ya kutupia picha ukiwa nusu utupu, hili ulilichu-kuliaje ukizingatia si maadili yetu kuachia picha kama zile?


Ramsey.

Idris: Ni maadili yetu kufanya kazi, kwa hiyo mimi pale nilikuwa kazini na suala hilo nililichukulia positive. Unajua hao wanaokutukana kwa wewe kufanya kazi, ukifulia wanakutukana pia. Huwezi kufanya kitu ukamfurahisha kila mmoja.

Showbiz: Unamzungumziaje Lulu ukizingatia umefanya naye kazi kwenye Tamthiliya ya Sarafu, kwa sasa ana takriban miezi mitatu gerezani, nini unachakusema?

Idris: Mungu atamsaidia atatoka. Ni kipindi kigumu kwake lakini pia hiki nacho kitapita.

Showbiz: Kupitia project yako ya Idris Foreman, umekuwa ukiwatania mpaka watu maarufu akiwemo rais, hufikirii kwamba hili linaweza kukupa tatizo?

Idris: Hapana mimi ni mchekeshaji, sasa kufanya utani na mtu yeyote haimaanishi ninamdharau. Ninawaheshimu viongozi wangu, ninafahamu pia wanapenda utani.

Showbiz: Mwisho kabisa una nini cha kuwaeleza mashabiki zako?


Idris: Kuna project nyingi nipo ninazipika, zikitoka itakuwa surprise kubwa, mashabiki wa kazi zangu wakae mkao wa kupokea.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Ni Kweri IDRIS Anateswa Na Kivuli Cha JOTI !
Ni Kweri IDRIS Anateswa Na Kivuli Cha JOTI !
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZ-Uh02uP5w2X6sb-6cKG7fWOxfsmjq1-vHsD3VWMwimUbXb7UQrHlOqsSZ0CXle1yauoaiqAL2ClbQDPArYs5KKw8CbGaomP2CZfZKkrTbCaI2Edt7WY1Qe-36U536gwrA80fpkJQwq7w/s640/Idris-Sultan-7.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZ-Uh02uP5w2X6sb-6cKG7fWOxfsmjq1-vHsD3VWMwimUbXb7UQrHlOqsSZ0CXle1yauoaiqAL2ClbQDPArYs5KKw8CbGaomP2CZfZKkrTbCaI2Edt7WY1Qe-36U536gwrA80fpkJQwq7w/s72-c/Idris-Sultan-7.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/ni-kweri-idris-anateswa-na-kivuli-cha.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/ni-kweri-idris-anateswa-na-kivuli-cha.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy