RAIS MAGUFULI Asitisha Mpango Wa Kuwasaidia Wakimbizi

Wakimbizi wa Burundi Tanzania inasema inajiondoa katika mpango wa Umoja wa mataifa wa kuwasaidia wakimbizi kuanza maisha mapya k...


Wakimbizi wa Burundi


Tanzania inasema inajiondoa katika mpango wa Umoja wa mataifa wa kuwasaidia wakimbizi kuanza maisha mapya katika mataifa yanayowahifadhi.

Tanzania limekuwa eneo salama kwa wakimbizi wengi na sasa inahifadhi zaidi ya wakimbizi 250,000 wa Burundi ambao walitoroka kwao ktutokana na matatizo katika nchi yao.


Rais John Pombe Magufuli amesema kwamba taifa lake linajiondoa kutokana na tatizo la usalama pamoja na lile la kifedha .
Mwaka uliopita taifa hilo lilisimamisha kwa muda usajili wa wakimbizi wapya na kuwataka wakimbizi wa Burundi kurudi nyumbani , hatua ambayo ilishtumiwa na makundi ya kupigania haki za kibinaadamu.

Kitengo hicho cha Umoja wa Mataifa kinasema kuwa kinatuma ujumbe wa ngazi za juu kwa mazungumzo na serikali ya Tanzania.
Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la wakimbi la Umoja wa Mataifa UNHCR.
Ripoti hiyo anasema hadi hivi sasa, kuna wakimbizi Laki 2 na elfu 41 kutoka Burundi wanaopatiwa makazi nchini Tanzania.

Katika idadi hii kubwa ya watu wanaokimbia nchi yao, UNHCR inasema asilimia 60 ni watoto.
Na ndani ya kipindi cha miezi mitano tu ya mwaka huu wa 2017, wakimbizi 44,487 wamekimbia Burundi na kuingia Tanzania

UNHCR inasema huu ni mzigo mkubwa kwa Tanzania lakini kwa bahati mbaya, nchii hii haipati fedha za kutosha kuwahudumia wakimbizi na wengine wanaotafuta hifadhi
Kambi moja kwa mfano ya Nyarugusu, ambayo inatajwa kuwa ni moja ya kambi kubwa za wakimbizi duniani, inahifadhi wakimbizi 139,0000 idadi ambayo inapaswa kupunguzwa na kuwagawa wakimbizi katika kambi nyingine.

Lakini hili limeshindikana, ripoti ya UNHCR inasema, na ni kwasababu ya kukosekana kwa ardhi ya kufungua kambi mpya

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: RAIS MAGUFULI Asitisha Mpango Wa Kuwasaidia Wakimbizi
RAIS MAGUFULI Asitisha Mpango Wa Kuwasaidia Wakimbizi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSffY-ngrmpYFYIi452y7QVrjIFriwcwd0574GxTZNF_Q4YXcXf5Kt7O1096wgXPSvtefzDxhdaGaiMYe7zZ27W8RfQActmI8j0MCsBqMlrhhjryyofFk3iB-fkf3eUKLcU3pyOmL8skRd/s640/kimbizi.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSffY-ngrmpYFYIi452y7QVrjIFriwcwd0574GxTZNF_Q4YXcXf5Kt7O1096wgXPSvtefzDxhdaGaiMYe7zZ27W8RfQActmI8j0MCsBqMlrhhjryyofFk3iB-fkf3eUKLcU3pyOmL8skRd/s72-c/kimbizi.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/rais-magufuli-asitisha-mpango-wa.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/rais-magufuli-asitisha-mpango-wa.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy