Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe akionesha picha ya marehemu. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema ...
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe akionesha picha ya marehemu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na
Mawasiliano CHADEMA, Tumaini Makene imeeleza kuwa mwili wa marehemu
Daniel unatarajiwa kufika nyumbani kwake Hananasif, ukitokea hospitali
ya Taifa Muhimbili majira ya saa 4 asubuhi na kisha kupelekwa katika
Kanisa la Katoliki la Kwa Pinda kwa ajili ya misa ya kumuombea marehemu
itakayoanza saa 5 asubuhi kanisani hapo.
Baadaye, waombolezaji watatoa heshima zao za mwisho kwa Daniel kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda mkoani Iringa ambako atazikwa siku ya Jumatano, katika kijiji cha Chikelewatu wilayani Mafinga.
COMMENTS