Ripoti ya uchunguzi wa mwili wa Akwilina aliyepigwa risasi yatoka

Madaktari wa hospitali ya Muhimbili Jumanne hii mchana wamefikia uamuzi wa kutoa sehemu ya ripoti ya uchunguzi wa mwili wa Mwanafunzi wa...


Madaktari wa hospitali ya Muhimbili Jumanne hii mchana wamefikia uamuzi wa kutoa sehemu ya ripoti ya uchunguzi wa mwili wa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyepigwa risasi na Polisi Februari 16, 2018.

Hatua hiyo imekuja baada ya ndugu wa binti huyo kususa kupokea mwili wa mwanafunzi huyo uliokuwa ukifanyiwa uchunguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) bila kuelezwa nini kilichomuua.

Wakizungumza mara baada ya maafikiano baina yao na madaktari, wamesema sehemu ya ripoti ya uchunguzi ambayo wameridhika nayo na sasa wanakwenda kufanya kikao cha ndugu kujadili namna gani watampumzisha Akwilina.

Shemeji wa mwanafunzi huyo, Festo Kavishe amesema uchunguzi wa mwili huo, umeonyesha kwamba Akwilina alijeruhiwa vibaya kichwani.
“Ripoti ambayo tumepewa imeonyesha kwamba kichwa cha marehemu kilipasuliwa vibaya na risasi ambayo iliingilia upande wa kushoto kwa kichwa chake na kutokea upande wa kulia ambao umefumuka vibaya,” amesema.

Kwa mujibu wa Kavishe, iwapo madaktari wasingewapatia majibu hayo wasingethubutu kuuchukua mwili huo kwa mazishi, kwa sababu walihitaji kupata picha kamili ya nini kilimuua Akwilina.
“Sasa tumeshafahamu nini hasa kimemuua ndugu yetu kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na madaktari baada ya uchunguzi, hivi sasa tunakwenda kujadiliana kuhusu mazishi yake,” amesema Kavishe.


Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Ripoti ya uchunguzi wa mwili wa Akwilina aliyepigwa risasi yatoka
Ripoti ya uchunguzi wa mwili wa Akwilina aliyepigwa risasi yatoka
https://1.bp.blogspot.com/-S3sNIq35-P0/WovfdUvKhdI/AAAAAAAACjo/Ebx6LSrcXVgZ9HfRZPPcphWcE7-ePXmkwCLcBGAs/s640/Engine-.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-S3sNIq35-P0/WovfdUvKhdI/AAAAAAAACjo/Ebx6LSrcXVgZ9HfRZPPcphWcE7-ePXmkwCLcBGAs/s72-c/Engine-.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/ripoti-ya-uchunguzi-wa-mwili-wa.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/ripoti-ya-uchunguzi-wa-mwili-wa.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy