Serikali Yahamasisha Kilimo Cha Mazao Makuu Matano

Serikali inaendelea na mpango wa kuhamasisha ulimaji wa mazao makuu matano ya Pamba, Korosho, Tumbaku, Kahawa na Chai nchini ili kuongez...


Serikali inaendelea na mpango wa kuhamasisha ulimaji wa mazao makuu matano ya Pamba, Korosho, Tumbaku, Kahawa na Chai nchini ili kuongeza uzalishaji wa mazao hayo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameyasema hayo Bungeni Mjini Dodoma wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Sumve Mhe. Richard Ndassa juu ya namna Serikali ilivyojipanga na utafutaji wa masoko ya Pamba kutokana na mwitikio mkubwa wa kulima zao hilo mwaka huu.

“Miongoni mwa mikakati ya kuendeleza mazao hayo ni pamoja na kulima kisasa na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi,” alisema Waziri Mkuu.
Amesema, mwezi huu anatarajia kukutana na watumiaji wa zao la Pamba hapa nchini ili kuweka mfumo endelevu wa ununuzi wa zao hilo. Aidha, Wizara ya Kilimo inafanya kazi ya kutafuta masoko nje ya nchi.

Pia, Mhe. Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi Kuchauka juu ugawaji wa pembejeo za korosho kwa mwaka huu amesema, Serikali ilitoa pembejeo ya Salfa bure mwaka jana kwa wakulima wa korosho ili kufanya hamasa kwa zao hilo baada ya wakulima kutelekeza zao hilo kutokana na kukosa pembejeo hiyo.

“Baada ya ugawaji wa pembejeo hiyo ya Salfa zao hilo limevunwa kwa kiwango cha juu kwa mwaka jana, hivyo kutokana na fedha walizozipata wakulima wa zao hilo watatatikiwa kuchangia gharama za Salfa kwa mwaka huu,” alisema Mhe. Majaliwa.


Wakati huo huo, Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Urambo Mhe. Margaret Sitta juu ya migogoro ya mipaka ya mapori na misitu, amesema Serikali imeiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikisha wanavijiji na viongozi wa kijiji wakati wa uwekaji wa mipaka hiyo.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Serikali Yahamasisha Kilimo Cha Mazao Makuu Matano
Serikali Yahamasisha Kilimo Cha Mazao Makuu Matano
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhevV-EBm_JJjHfnxJFZe1RWFlS_jfYgNrWzejkPruL819D6iplQzNDBpigwa85SHcTSeikmsbV0lMJ79qdBF91u5TGMVdzkbxduoQaVzmEGCkWtGvz3YSYRYiu8y7redVoUbHAuSw7S3P_/s640/makuu.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhevV-EBm_JJjHfnxJFZe1RWFlS_jfYgNrWzejkPruL819D6iplQzNDBpigwa85SHcTSeikmsbV0lMJ79qdBF91u5TGMVdzkbxduoQaVzmEGCkWtGvz3YSYRYiu8y7redVoUbHAuSw7S3P_/s72-c/makuu.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/serikali-yahamasisha-kilimo-cha-mazao.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/serikali-yahamasisha-kilimo-cha-mazao.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy