Kaimu Mkurugenzi wa TFDA, Agnes Kijo Serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Tanzania (TFDA) kwa kushirikiana na Jeshi ...
Kaimu Mkurugenzi wa TFDA, Agnes Kijo
Akizungumza na waandishi wa habari jana Februari 18, 2018 jijini Dar
es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa TFDA, Agnes Kijo amesema matangazo hayo
yanatakiwa kukoma mara moja na wahusika wanastahili kufika katika
mamlaka hizo kuomba kibali.
Amesisitiza kuwa matangazo ya vipodozi na dawa hizo yamekuwa na madai mbalimbali kama vile kuongeza makalio, kuongeza nyonga, sehemu za siri za mwanaume, kurudisha bikira kwa wanawake na kuondoa mabaka sugu na dawa hizo zipo kwenye mfumo wa vidonge, jeli, losheni, mafuta, krimu na dawa za kunywa. Kijo alisema baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha umma kuwa bidhaa zao zimethibitishwa na TFDA kitu ambacho si kweli.
COMMENTS