Shehe Alhadi akizungumza na wanahabari katika mkutano huo. SHEHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa amemuonya mwanahar...
Shehe Alhadi akizungumza na wanahabari katika mkutano huo.
SHEHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa amemuonya mwanaharakati maarufu, Mange Kimambi kwa madai kuwa amemporomoshea matusi mazito baada ya kumuona mtandaoni amepiga picha na mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maulid Mtulya.
Mufti akiwasili ofisi za Bakwata mkoa wa Dar kushoto ni Shehe Alhadi.
Shehe Alhadi ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa picha hiyo alipiga na mgombea huyo baada ya kukutana msibani ndipo baadhi ya wanachama wa CCM waliomba kupiga nae picha jambo ambalo asingeweza kulikataa alisema Alhadi.
Mange Kimambi.
Alhadi akimkaribisha Mufti ofisini kwake na kisha kumshitakia ishu ya Mange Kimambi.
Mufti akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
“Kama amezoea kuwatukana viongozi wa serikali asituchezee viongozi wa kidini, ulimi na mikono aliyopewa na Mwenyezi Mungu hakupewa kwa ajili ya kuwakashifu watu hivyo hapa alipochokoza sasa ameingia sipo, nasema mwaka huu hataumaliza salama.,” alisema Shehe Mussa.
Mkutano huo ukiendelea hawa nao wakisikiliza.
Baada ya kusema hayo, Shehe Alhadi alimkaribisha, Mufti Abubakar Zuberi aliyemtembelea ofisini kwake akiwa kwenye ziara za kutembelea ofisi za Bakwata nchi nzima na kuwahimiza waislamu wote kuitambua na kuiunga mkono taasisi hiyo na kuepuka migogoro.
Mkutano huo ulimalizwa kwa duwa.
Hapa ndipo ulipofanyika mkutano huo.
Alhadi akiweka mambo sawa wakati Mufti akitaka kuondoka.
COMMENTS