Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoa wa Dar es Salaam Macdonald Maganga akitoa uamuzi wa wao kuwaweka kampuni ya u...
Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoa wa Dar es Salaam Macdonald Maganga akitoa uamuzi wa wao kuwaweka kampuni ya udalali ya Yono Auction kwa ajili ya kwenda kukamata wadaiwa sugu wote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, Scholastica Kevela akitoa tamko la siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), kulipa madeni yao kabla ya chukuliwa hatua za kisheria ikiwamo mali zao kupigwa mnada kufidia deni.
Meneja wa SIDO mkoa wa Dar es Salaam Macdonald Maganga akiongoza wafanyakazi na viongozi wa Yono kupita mlango kwa mlango wakati wakizundua kampeni ya kudai madeni "LIPA DENI LAKO SIDO, KUWA MZALENDO'.
Wakiingia katika moja ya ofisi za mdaiwa wa SIDO.
Nae Mwenyekiti wa Kuatamia mawazo ya wabunifu, Joseph Mlay ameiunga
mkono SIDO kwa hatua waliyochukua ya kuingia mlango kwa mlango katika
kudai madeni yao.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), mkoa wa Dar es Salaam
imetangaza vita kwa wale wadaiwa sugu kulipa madeni yao kabla ya
chukuliwa hatua za kisheria ikiwamo mali zao kupigwa mnada.
Kauli hiyo ameitoa jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Shirika la
Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), mkoa wa Dar es Salaam Macdonald Maganga
wakati akizindua kampeni ya kukusanya madeni kwa wateja wao.
"Leo tunazindua kampeni ya kukusanya madeni kwa wadaiwa sugu wote wa
SIDO hatutakuwa na huruma juu ya hili maana hawa ndiyo wanarudisha
maendeleo ya shirika nyuma, kuna waliokopa, walipanga kama haujalipa
deni lako ujue tunakupa siku 14 tu baada ya hapo sheria itachukua mkondo
wake," amesema Mkurugenzi Maganga.
Meneja Macdonald Maganga amesema wadaiwa ni wale waliopewa maeneo
maalumu ya viwanda kwa ajili ya kufanyia kazi zao na waliopatiwa huduma
ya fedha kwa mkopo na kushindwa kurejesha kwa wakati.
“Kuna ambao wamekaa miaka mingi au miezi mingi bila kurejesha fedha
kwetu kama shirika inatuathiri kwa sababu hatuwezi kuwahudumia wengine,”
amesema Maganga.
Maganga amesema wanadai jumla ya sh. milioni 350 kutoka kwa wadaiwa zaidi ya 77.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono Auction
Mart, Scholastica Kevela amewashukuru SIDO kwa kuweza kuwapa kazi hiyo
ya kuwakusanyia madeni na kuongeza kuwa hawata muonea huruma mdaiwa
yeyote.
"Yono Auction Mart tunatoa siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Shirika la
Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), kulipa madeni yao kabla ya chukuliwa
hatua za kisheria ikiwamo mali zao kupigwa mnada kufidia deni,". amesema
Mama Kevela.
“Kwa wadaiwa wote wa SIDO, wanaoishi kwenye viwanda na nyumba za SIDO
bila kulipa pango, waliochukua mikopo na hawataki kurejesha kwa sababu
wanazozijua wao, mkono wa Yono uko kazini ni vyema wakachukua hatua
wakalipa ili kuondosha usumbufu,” amesema Kevela.
Mdaiwa Masoud amedai hawafanyi makusudi kutolipa madeni ni kutokana na
kodi kupanda kila mwaka huku hali ya biashara ikiwa mbaya.
“Ukizingitia soko la ushidani na hali ya bidhaa unashindwa kuuza kwa
wakati kwa hiyo tunalipa lakini hatulipi kwa wakati,” amesema.
Amedai wamepangishwa kwa zaidi ya miaka 40 wakifanya shughuli zao na
kama wangekuwa hawalipi kwa kipindi chote wangefukuzwa hivyo ameiomba
serikali kutodhani kuwa wanapuuza kulipa madeni.
COMMENTS