Wakati wabongo wakiendelea kumshambulia mitandaoni kwa aina ya mtindo wa kupaka rangi za kijani kwenye nywele zake, Msanii Ben Pol amene...
Wakati wabongo wakiendelea kumshambulia mitandaoni kwa aina ya mtindo wa kupaka rangi za kijani kwenye nywele zake, Msanii Ben Pol ameneemeka na staili hiyo kwani ameshalamba dili nono na kampuni ya Green Telecom inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na IT.
Ben Pol akitia saini baadhi ya nyaraka na Viongozi wa Green Telecom Tanzania.
“Ni kweli nimepata dili nzuri yenye mkataba kabisa na Green Telecom lakini kwa sasa bado kuna vitu vinamalizika halafu tutatoa taarifa kamili na wenyewe ila ni dili kubwa,“amesema Ben Pol.
Huu ni muendelezo wa mafanikio kwa Ben Pol kwani mwishoni mwa mwaka jana alipata dili kadhaa ikiwemo ya ubalozi wa MAÜA association.
COMMENTS