TLS: Wampa Kauli Ngumu Rais Magufuli

Makala hii ni sehemu iliyokuwa imebaki wiki iliyopita katika risala iliyohaririwa ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Tanga...


Makala hii ni sehemu iliyokuwa imebaki wiki iliyopita katika risala iliyohaririwa ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Godwin Ngwilimi,  katika maadhimisho ya siku ya Sheria nchini, Endelea……………….

Majukumu hayo ni pamoja na kusimamia na kuboresha kiwango cha mienendo ya elimu ya sheria kwa Tasnia ya sheria nchini; kusaidia upatikanaji wa elimu ya sheria kwa wanachama wa jumuia ya mawakili; kuishauri na kuisaidia Serikali, mahakama katika masuala yote yahusuyo sheria; kuwakilisha, kuwalinda na kuwasaidia wanachama katika Tasnia ya sheria kuhusu hali ya kutoa huduma ya sheria na mengineyo; kulinda na kusaidia wananchi wa Tanzania katika masuala yote yahusuyo sheria na mengineyo yenye mlengo wa sheria na kwa ujumla kuratibu masuala yote yahusuyo tasnia ya sheria kwa upande wa Tanzania Bara.

Sisi kama washauri wa serikali kisheria tumekuwa na changamoto kadha wa kadha ambazo tungependa kushiriki kikamilifu katika kuzitatua tukishirikiana na wadau wetu kwa pamoja. Changamoto nyingi ambazo tungependa tuzifanyie kazi ili kuendana na kasi ya maendeleo inayosukumwa na matumizi ya Tehama inayotajwa na kauli mbiu hii ni pamoja na hizi zifuatazo katika makundi makuu matatu:

Changamoto  ya mafunzo darasani na vitendo ya elimu ya sheria kwa ujumla kulingana na maendeleo ya kisheria katika mambo mengi mapya yanayoibuka;
  • Changamoto ya huduma zetu za sheria kwa wananchi, leseni za uwakili na kuibuka kwa vishoka wanaoingilia uanachama wetu, hali ya uanchama wetu kuepuka migogoro ya masilahi; na
  • Changamoto ya maadili na nidhamu ya mawakili kwa ujumla na watoa huduma ya sheria.
Ni ukweli usiofichika kwamba mafunzo ya sheria ya darasani na yale ya vitendo yana changamoto ya kutoendana  au kuendana na taratibu na mahitaji makubwa ya kitaifa yanayoibuka hivi sasa kwa kasi kubwa.
Tunashudia kukua kwa kasi ya mambo Tehama, mafuta na gesi, utakatishaji fedha, madawa ya kulevya, kuwepo kwa bidhaa feki zinazohatarisha afya na uchumi wa walaji, ushindani wa kidunia, kimataifa wa makampuni ya kibiashara.

Nyingine ni biashara  zinazopitia angani na ng’ambo ya nchi, biashara za kibhari, maji na maziwa; na kadharika kadharika. Changamoto hizi zinalazimu, sio tu kujaza wanafunzi wa sheria darasani katika vyuo vyetu vya kawaida bali kutengeneza vyuo mahususi bobezi, wataalamu maalumu waliofuzu vizuri kinadharia na kivitendo ili wawe waalimu, wanasheria, mawakili na watendaji kukabiliana na hali hii kwa haraka.

Hali kadhalika, huduma yetu ya sheria kutoka kwa wanachama  wetu inazidi kushuka kwa kasi ikitokana na kukosa uwezo wa kitaaluma (professional competency), kushuka kwa heshima na hadhi ya wakili  kulingana na ukubwa wao (seniority) na kuonekana wazi katika mahakama na jamii kwa ujumla; kuongezeka kwa mashauri yanayotokana na kushindwa kutoa huduma bora kwa wateja dhidi ya mawakili mbele ya vyombo vya mahakama na baraza la mawakili; kushuka kwa imani ya wananchi kuhusu huduma za kisheria; mmonyonyoko wa miiko ya uwakili inayosukumwa na ushindani wa kujitajilisha; kudhoofu kwa vyombo vya usimamizi wa mawakili na kutokuwa na adhabu sitahiki kwa wenzetu wanaokiuka miiko iliyopo.

Na changamoto ya tatu ni hii ya kushuka kwa maadili ya mawakili mbele ya jamii ikiwa ni pamoja na mbele ya vyombo vya utoaji haki, utawala, watawala na mamlaka za kutunga sheria; na kupitwa kwa wakati au kuwa nyuma au kutojitoshereza kwa sheria; kukosekana au kuwa na kanuni dhaifu na vyombo vya usimamizi wa nidhamu kulea na kuadabisha mienendo ya mawakili. Si kitu cha ajabu kabisa hivi kusikia mwananchi akishangaa, kujiuliza na kupigwa bumbuwazi kwa kusema kuwa; “huyu naye ni wakili !!!?”

Changamoto hizi kwetu sio kitu kidogo hata kidogo. Tulishaziona na tunaziona zikikua kila iitwapo leo. Zinatutia aibu na kupaka matope taaluma yetu ambayo  imetupatia dhamana ya kutoa haki. Sisi jumuiya ya mawakili Tanzania Bara  tulishaomba na kuanzisha mchakato wa ndani wa kupitia na kufanya  mabadiliko makubwa mfano wa Tasnia ya sheria. Juhudi zetu zilianza tangu miaka ya 2007 tukitaka kuona sheria ya mawakili, sheria na vipengele vya elimu ya sheria kinadharia na matendo, sheria ya jumuiya yetu zikifanyiwa marekebisho kukidhi mahitaji ya hali sasa ya kimaendeleo na kurudisha heshima ya tasnia yetu ya sheria.

Kwa sababu za kimsingi na kwa manufaa ya taifa letu, tutafarijika sana sana Mheshimiwa mgeni rasmi kama utatoa Baraka zako za kuundwa chombo cha pamoja kitakachogusa au kuwakilisha tasnia yote ya sheria ili iwezo kukaa chini na kukusanya mapendekezo yatakayojibu hoja na haja zilizopo  sasa hivi. Kwetu sisi kama jumuiya ya mawakili, tuko tayari kabisa kushiriki kwa namna yeyote (hali na mali) na vyombo na tasisi zingine za umma na binafsi katika tasnia ya sheria, kama itakupendeza, kuongoza mchakato huu.

Nimalizie kwa kukufahamisha kuwa tulishaanza ujenzi wa jengo la mawakili lijulikanalo kama Legal Aid Advocacy Centre (LAAC) ambalo linatumika kubeba ofisi zetu za Dar es Salaam, kutoa huduma za msaada wa sheria, kutoa mafunzo ya ubobezi katika matendo (legal specialization) kupitia kamati yetu ya elimu endelevu kwa mawakili na kufanya usuluhishi wa mashauri (ADR). Mheshimiwa mgeni rasmi, tutumie wasaa huu kukuomba, pale utakapopata nafasi uje uweke Baraka zako.

Hali kadhalika, tunaungana na kauli mbiu yako ya kuhamia Dodoma. Tayari tumeanza kwa kukodisha ofisi Dodoma kuweka ofisi yetu kule ili kuwa karibu na wadau wetu ambao ni serikali, Bunge na Mahakama katika kutoa huduma kwa wananchi. Hata hivyo, mtazamo wetu mkubwa ni kupata kiwanja kitakachowezesha kujengwa kwa jengo na ukumbi mkubwa kwa ajili ya mikutano yetu na wanachana  ikiwa ni pamoja  na wadau wetu.


Kama kauli mbiu ya maadhimisho hayo inavyosema “Matumizi ya Tehama katika Utoaji Haki kwa wakati na kwa kuzingatia Maadili” ni kichocheo muhimu katika utoaji haki kwa haraka na kwa wakati. Tunapenda kuishukuru Mahakama kwa mwaliko huu wa kushiriki siku hii muhimu kwetu sisi wadau ambao ndio msingi wa utoaji haki na usawa kwa wakati katika jamii.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: TLS: Wampa Kauli Ngumu Rais Magufuli
TLS: Wampa Kauli Ngumu Rais Magufuli
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhfa2c32WpkWzlLAAohmKZHwwF_tBlQ5ciRIhPQ1D6gyWrxpL_fLDg95FDXBMTMbufArGDEaOdH0Didy2NnavvfvI8-3vw425Lh3he7fJv2CcA8JYq0e6fg0JDhRYtbsxTYkfoxhJWFXVRb/s640/tcl.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhfa2c32WpkWzlLAAohmKZHwwF_tBlQ5ciRIhPQ1D6gyWrxpL_fLDg95FDXBMTMbufArGDEaOdH0Didy2NnavvfvI8-3vw425Lh3he7fJv2CcA8JYq0e6fg0JDhRYtbsxTYkfoxhJWFXVRb/s72-c/tcl.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/tls-wampa-kauli-ngumu-rais-magufuli.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/tls-wampa-kauli-ngumu-rais-magufuli.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy