Tumekuwa Binadamu - Washangilia Wanawake Saudi Arabia Kwa Kuingia Uwanjani

Hatimaye wanawake nchini Saudi Arabia wameingia kwa mara ya kwanza kwenye viwanja vya mpira kushuhudia mchezo huo pendwa zaidi duniani. ...


Hatimaye wanawake nchini Saudi Arabia wameingia kwa mara ya kwanza kwenye viwanja vya mpira kushuhudia mchezo huo pendwa zaidi duniani.


Wanawake hao waliohudhuria kwenye mchezo wa Derby ya Ryadh kati ya Al-Nassir FC na Al-Hilal FC kwenye Uwanja wa Taifa wa King Fahad wikiendi iliyopita walionekana wenye furaha huku wengi wakiimba kuwa wamekombolewa na wamekuwa binadamu wa kawaida kama wanawake wengine duniani.

Wanawake hao ambao waliongozwa na mwanaharakati  Madeha al Ajroush (63) ambaye ndiye amekuwa akipigania haki za wanawake kuingia viwanjani na kuendesha magari tangu akiwa na miaka 18, amesema ni furaha kuona malengo yake yamekamilika ingawaje umri umemtupa mkono.

Tangu nikiwa na miaka 18 nilijua itafika muda wanawake tutaendesha magari na kuingia kwenye viwanja na kweli imetimia ingawaje hatua imechelewa hadi sasa nina miaka 63 lakini imenipa funzo katika maisha yangu,“amesema Bi. Al Ajroush ambaye amefungwa zaidi ya mara tatu akipigania usawa wa kijinsia nchini Saudi Arabia.


Wanawake wengine walioonekana uwanjani hapo walisikika wakiimba na kushangilia kwa furaha sio kwa sababu ya mpira bali kutokana na kuruhusiwa kuingia viwanjani.

Tunajiona kama tumekuwa binadamu kwa sasa kwani tunaweza kujiamulia kipi cha kufanya na sio kuamuliwa na mtu kama ilivyo kuwa awali,“amesikika Mwanafunzi wa kike wa miaka 18 kwenye mahojiano na Sky News.

Hatua hiyo imekuja baada ya baada ya mwaka jana nchi hiyo kuruhusu wanawake kuendesha magari na kuanza kuingia viwanjani kuanzia mwaka huu.

Awali wanawake nchini humo walikuwa hawaruhusiwi kuingia viwanjani lakini kuanzia mwaka huu wataingia kwenye viwanja vya michezo kwa masharti ya kujifunga Hijab na Niqab.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Tumekuwa Binadamu - Washangilia Wanawake Saudi Arabia Kwa Kuingia Uwanjani
Tumekuwa Binadamu - Washangilia Wanawake Saudi Arabia Kwa Kuingia Uwanjani
https://1.bp.blogspot.com/-IK1SZu_SWsg/WoKp0L2MPwI/AAAAAAAACMA/rpBHvCvnp8wSPLCdVdfRmzQXGwqecJwdACLcBGAs/s640/ud%2B1.PNG
https://1.bp.blogspot.com/-IK1SZu_SWsg/WoKp0L2MPwI/AAAAAAAACMA/rpBHvCvnp8wSPLCdVdfRmzQXGwqecJwdACLcBGAs/s72-c/ud%2B1.PNG
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/tumekuwa-binadamu-washangilia-wanawake.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/tumekuwa-binadamu-washangilia-wanawake.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy