Kundi la Muziki la Shiikane linaloundwa na wasanii watatu kutoka Nigeria, HrH Shay, Princess Annamay na Baby-K, linatarajia kutua nchin...
Kundi la Muziki la Shiikane linaloundwa na wasanii watatu kutoka Nigeria, HrH Shay, Princess Annamay na Baby-K, linatarajia kutua nchini Tanzania mwaka huu kwaajili ya kufanya media tour pamoja na kufanya promotion ya wimbo wao mpya ‘Oga Police’.
Mrembo hao ambao makazi yao ni Uingereza na Nigeria wanafanya kazi chini ya label M.A Records na wameandaa kampeni yao ya #ogapolice#tanzaniatour kwaajili ya kutoa zawadi mbalimbali za hela kwa washindi nchini Tanzania.
Shiikane ambao ni washindi wa tuzo ya BEFFTA Awards 2015 – Best Music
Video kupitia video yao ya wimbo ‘Tuele’ wanaonekana kuwa ni kundi la
wasanii wa kike ambalo linakuja kwa kasi zaidi barani Afrika.
Wakali hao wa kuimba ambao kwa sasa wanafanya vizuri na video ya wimbo ‘Oga Police’ wanakuja Tanzania baada ya kuona kuna mashabiki wengi wanaoufuatilia muziki wao kwa ukaribu zaidi.
Wasanii hao wamewataka mashabiki wa muziki nchini Tanzania kujirekodi
clips za video wakicheza wimbo ‘Oga Police’ na then kuzituma whatsapp
kwa mamba 0785272727 ili kujishindia zawadi mbalimbali.
Pia warembo hao wakija Tanzania watafanya jitihada za kufanya kolabo na wasanii wa ndani ili kupata ladha tofauti katika muziki wao.
COMMENTS