Tupo katika mwaka 2018 Wanasayansi wanaendelea kuonesha kuwa Teknolojia inakuwa mtu wangu, kutoka Uingereza siku za hivi karibuni wataa...
Tupo katika mwaka 2018 Wanasayansi wanaendelea kuonesha kuwa Teknolojia
inakuwa mtu wangu, kutoka Uingereza siku za hivi karibuni wataalamu
kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh, wameeleza kuwa yai la binadamu
(mwanamke) linakuzwa katika maabara kwa mara ya kwanza duniani.
Wataalamu hao wanaeleza kuwa Teknolojia hii mpya itasaidia kuvumbua njia
mpya za kuhifadhi uzazi wa watoto ambao wako kwenye matibabu ya
magonjwa ya saratani na pia ni fursa ya kuchunguza jinsi yai la binadamu
linavyokua jambo ambalo milele yote limekuwa siri kwa sayansi.
Inaelezwa kuna imechukua miaka mingi ya kufanyia kazi teknolojia hiyo na
hata walipofikia bado haijaweza kuanza kutumika rasmi na kwamba
wataalamu sasa wataweza kukuza yai la mwanamke hadi kukomaa kabisa
likiwa nje ya ovari.
COMMENTS