Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia tiketi ya CHADEMA, John Heche ameweka wazi kuwa kwa sasa ameanza kupata vitisho mbalimbali kutoka kwa w...
Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia tiketi ya CHADEMA, John Heche ameweka wazi kuwa kwa sasa ameanza kupata vitisho mbalimbali kutoka kwa watu wasiojulikana wakimtishia kumpoteza baada ya kusema ukweli kuhusu kupanda kwa gharama za vitambulisho vya Taifa.
Mhe. John Heche
Mhe. Heche amesema vitisho hivyo vimekuja baada ya kutoa taarifa Bungeni kuwa serikali ilidanganya umma juu ya mradi wa e-passports na kupanda kwa gharama za vitambulisho vya Taifa.
Soma taarifa yake kamili hapa chini aliyoitoa kwa Vyombo vya Habari;
Vitisho dhidi yangu kuhusu mradi wa e-passports na vitambulisho vya Taifa:
Mtakumbuka kuwa juzi jioni nilizungumza bungeni kuhusu Serikali
kudanganya umma Kuhusu mradi wa e-passports na kuhusu kupanda kwa
gharama za vitambulisho vya Taifa. Maelezo yangu bungeni yalitokana na
Taarifa kutoka Kamati ya PAC na yalijibiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani
ya nchi.
Sasa ndugu zangu nimeanza kupata vitisho dhidi ya ‘credibility’ yangu na
maisha yangu. Ndugu zangu Taifa letu linapitia wakati ngumu Sana.
Genge la wahalifu wa ki Uchumi na kisiasa kamwe lisitarajie nitatishika
ama kubadili msimamo. Vitisho vilivyoanza dhidi yangu baada ya kuibua
Ufisadi Katika Vitambulisho vya Taifa na E -Pasport havitaniogopesha
kamwe. Njia zao ovu AMA kunitisha ama kutaka kuchafua Heshima yangu AMA
kunitengenezea kesi AMA kuninifanyia alichofanyiwa mh Tundu Lisu
hazitanirudisha nyuma. Leo nimepigiwa simu kipeperushi kinachojiita
gazeti la Tanzanite kwa kutumia namba ya simu 0713295860 kusema eti
nimehongwa ili kuzungumza nilichozungumza Bungeni. Hizi ni njama za
kizamani kufunga watu midomo.
Ninahitaji mambo 2 tu, moja Serikali ionyeshe kuwa ilitoa kazi ya
e-passports kwa zabuni na washindani walikuwa kina nani. Pia alichosema
Rais ni kwa components zote 6 za mradi au ni kwa passport tu? Mbili,
Serikali iweke wazi nyongeza ya mkataba ya vitambulisho vya Taifa na
ieleze sababu za gharama ya kutengeneza kitambulisho kupanda kutoka
shilingi 17,000 kwa kitambulisho Mpaka shilingi 26,000 kwa kitambulisho.
Serikali iache kunitisha. Naandaa nyaraka zote muhimu na nitapeleka
Bungeni kuomba Kuundwa Kamati Teule ya kibunge juu ya ubadhirifu huu.
Serikali itambue kuwa rasimu ya Taarifa ya PAC iliyonyofoa Taarifa
kuhusu NIDA tunayo na tunajua njama zilizotumika kuondoa eneo hilo. Hata
nikiuwawa Watanzania watajua ukweli tu kwani Taarifa hiyo ipo kwa
wabunge wengi.
John Heche, Mb
Tarime Vijijini
3/2/2018
COMMENTS