Waziri Aagiza Watumishi 91 Watumbuliwe

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amemwagiza katibu Mkuu Wizara ya uvuvi Dk. Yohana Budeba pamoja na wakurugenzi wote wa halmashau...


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amemwagiza katibu Mkuu Wizara ya uvuvi Dk. Yohana Budeba pamoja na wakurugenzi wote wa halmashauri za wilaya katika mikoa ya kanda ya ziwa,Kuwafuta kazi mara moja watumishi 65 na viongozi wa kamati za usimamizi wa raslimali za uvuvi (BMU) 26 baada ya kubainika wanashiriki kufadhili uvuvi haramu ndani ya ziwa Victoria.

Akihitimisha operesheni maalum ya kitaifa ya kupambana na kudhibiti uvuvi na biasahara haramu ya mazao ya uvuvi katika ukanda wa Ziwa Victoria iliyodumu kwa siku 40, katika ukumbi wa chuo Kikuu cha benki jijini Mwanza, Mpina amesema operesheni hiyo itaendelea hadi disemba mwaka huu ili kuhakikisha uvuvi haramu unatokomezwa huku akidai hatasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayebainika kukwamisha juhudi za serikali.

Waziri Mpina pia ameonesha kuchukizwa na kitendo cha askari wa wanyamapori wa hifadhi ya kisiwa cha Lubodo mkoani geita kuwazuia watendaji wa kikosi cha operesheni hiyo wakati wa msako dhidi ya uvuvi haramu.


Operesheni hiyo ilianza Januari mosi mwaka huu, ambapo jumla ya wadau 1,200 waliopo kwenye sekta ya uvuvi nchini walikutwa na makosa mbalimbali na kutozwa faini ya shilingi Bilioni 4.7, huku tani 73 za samaki wasiokidhi kiwango wakigawiwa kwa wananchi,na tani 173 za mazao ya uvuvi zilitaifishwa,huku mali na zana mbalimbali za uvuvi zenye thamani kubwa ya fedha zikiteketezwa kwa moto.

COMMENTS

Name

Entertainment,110,Fashion,5,Health,5,Job,11,Lifestyle,2,Makala,6,Music,4,News,177,Sports,98,Videos,14,
ltr
item
Habari Today: Waziri Aagiza Watumishi 91 Watumbuliwe
Waziri Aagiza Watumishi 91 Watumbuliwe
https://1.bp.blogspot.com/-vl84jcYJcBE/WoKWSgVH1qI/AAAAAAAACHI/eXEGcatgdV442CZ3H8kDpIDgQUoq115JACLcBGAs/s640/mpina-1.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-vl84jcYJcBE/WoKWSgVH1qI/AAAAAAAACHI/eXEGcatgdV442CZ3H8kDpIDgQUoq115JACLcBGAs/s72-c/mpina-1.jpg
Habari Today
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/waziri-aagiza-watumishi-91-watumbuliwe.html
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/
http://habaritodaytzz.blogspot.com/2018/02/waziri-aagiza-watumishi-91-watumbuliwe.html
true
7010127043980995099
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy