Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART), Eng. Ronald Lwakatare (aliyesimama) akifafanua jambo kwa ujumbe wa Waziri wa Uje...
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi
yaendayo haraka (DART), Eng. Ronald Lwakatare (aliyesimama) akifafanua
jambo kwa ujumbe wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Lesotho
walipotembelea mradi huo.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Bw. Hija Malamla akizungumza
katika kikao cha pamoja kati ya wataalamu wa sekta ya barabara nchini na
ujumbe wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Lesotho uliko
nchini kwa ziara ya mafunzo.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi wa Lesotho, Mathabathe Hlalele (wa pili kulia) akisisitiza
jambo kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya ujumbe wa nchi hiyo
na Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi cha
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Bw. Lyanga (wa pili kushoto)
akiwasilisha mada kwa ujumbe wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali
ya Lesotho walipotembelea ofisi za TANROADS jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART), Eng. Ronald Lwakatare (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Moramotse (kulia) alipotembelea kukagua mradi huo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo
Moramotse (wa tatu kulia) akisisitiza jambo akiwa kwenye moja ya Mabasi
yaendayo haraka (DART) alipotembelea mradi huo jijini Dar es Salaam. Wa
pili kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART), Eng.
Ronald Lwakatare.
COMMENTS