Mshambuliaji wao Mzimbabwe, Donald Ngoma (kushoto) akifanya yake. YANGA ni kama wameshtukia janja ya mshambuliaji wao Mzimbabwe, D...
Mshambuliaji wao Mzimbabwe, Donald Ngoma (kushoto) akifanya yake.
Mshambuliaji huyo ambaye Simba walifikiria kumsajili mwanzoni mwa msimu huu, alipata majeraha hayo kwenye mechi ya nne ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Taarifa za uhakika ambazo Championi Jumatano imezipata kutoka ndani ya Kamati ya Utendaji ya Yanga na ile ya Mashindano ni kwamba zote zilikutana na wengi kuonyeshwa kukerwa hali ya Ngoma lakini wakakubaliana wapate faili lake la matibabu kwanza.
Habari zinasema wametoa siku mbili kuanzia leo Jumatano kwa ajili ya kufanyiwa vipimo chini ya daktari wa timu hiyo na baadaye ripoti ya majibu ya itakabadhiwa kwa mabosi wa timu hiyo ambao watafanya maamuzi. “Viongozi ni kama wamechoshwa na majeraha ya Ngoma ambayo yanakaribia miezi sita sasa hayajapona, hivyo viongozi wanahisi ni kama anawaongopea, wametoa siku mbili kwa ajili ya kumfanyia vipimo na ripoti kukabidhiwa kwa kamati hizo,”kilidokeza chanzo chetu.
Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati wa Mashindano na Usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema; “Sidhani kama ni sawa kuwa na mchezaji katika timu ambaye hana msaada halafu mwisho wa mwezi analipwa mshahara wa bure.”
“Kiukweli tulimvumilia kwa muda mrefu Ngoma, muda umefika sasa hivi kujua hatma yake na tayari tumemwambia daktari tunataka ripoti ya matibabu yake ndani ya siku mbili, hivyo anatakiwa kupelekwa hospitali ili kujua hatma yake, kama unavyojua kikosi chetu kinaandamwa na majeruhi wengi,”alisema Nyika.
Pia akinukuliwa Katibu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa jijini Dar es Salaam jana alisema: “Tunataka kuachana na wachezaji wenye majeraha ya muda mrefu kwa kuwa tumeona kuwa wanaiingiza klabu kwenye hasara kubwa, fedha hizo ni bora tufanyie kitu kingine,” Majeruhi wengine waliokuwepo kwenye kikosi hicho ambao nao watachunguzwa ni Youthe Rostand, Juma Abdul, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Haji Mwinyi, Pato Ngonyani, Yohana Nkomola, Andrew Vicent ‘Dante’, Thabani Kamusoko na Amissi Tambwe.
Wilbert Molandi, Dar es Salaam
COMMENTS